BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu.
Baada ya matokeo hayo kutangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, dkt. Charles Msonde, Global Publishers imefunga safari hadi Kunduchi jijini dar es Salaam ambapoilipo Shule ya Sekondari feza Boys ambayo imeshika nafasi ya pili Kitaifa na imetoa mwanafunzi wa sita Kitaifa katika matokeo hayo.
Baada ya kuwasili shuleni hapo tumebahatika kuonana na kufanya mahojiano na kinara huyo ambaye ni Fuad Thabit Thabit (17) ambaye ameeleza furaha yake kufuatia ushindi huo wa kihistoria kwake.
“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata matokeo haya. Jambo kubwa nililokuwa nikilifanya darasani ni kuwasikiliza vyema walimu wangu, kufanya juhudi na bidii zaidi katika masomo yangu, lakini kikubwa zaidi nilikuwa nikimtegemea Mwenyezi Mungu, niliamini na ninaamini ni Mungu pekee ndiye amebifanya niweze kufikia hapa niliopifika leo.
“Vile vile wazazi walikuwa ni nguzo kubwa kwangu katika kunitimizia mahitaji yangu ya shule, kunitia moyo na kunihimiza kuenenda katika maadili mema,” alisema Thabit.
Orodha ya Shule 10 Bora.
1. St. Francis Girls – Mbeya
2. Feza Boys – Dar es Salaam
3. Kemoboya – Kagera
4. Bethel Sabs Girls – Iringa
5. Anwarite Girls – Kilimanjaro
6. Marian Girls – Pwani
7. Canossa – Dar
8. Feza Girls – Dar
9. Marian Boys – Pwani
10. Shamsiye Boys – Dar
Shule Kumi (10) Za Mwisho Kitaifa
1. Kusini – Kusini Unguja
2. Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja
3. Mwenge SMZ – Mjini Magharibi
4. Langoni – Mjini Magharibi
5. Furaha – Dar
6. Mbesa – Ruvuma
7. Kabugaro – Kagera
8. Chokocho- Kusini Pemba
9. Nyeburu – Dar
10. Mtule – Kusini Unguja
PICHA NA DENIS MTIMA | GPL
Comments are closed.