The House of Favourite Newspapers

Bondia Mwanamke Aliyeamua Mpambano wa Mwakinyo & Mcongo

0

BAADA ya kumaliza kuamua pambano la ubingwa wa Dunia ‘WBF’ kati ya Mtanzania, Hassan Mwakinyo Tshibangu Kayembe kutoka DR Congo, mwamuzi mwanamke, Pendo Njau mapema asubuhi ya leo alitembelea  ofisi za Global Group katika kipindi cha Kick off kinachoruka kila Jumamosi kupitia +255Global Radio.

Njau ambaye aliambata na bingwa wa zamani katika ngumi za kulipwa, Japhet Kaseba  alisema kuwa haikuwa rahisi kwake kuweza kufikia mafanikio hayo kama asingekuwa Kaseba kwani ndiye alimshauri kuingia katika fani hiyo baada ya kuachana na mchezo wa Kick Boxing.

Mbali ya hayo mwamuzi huyo amefichua kuwa kijiamini kwake ndiyo kumepelekea kuweza kulimudu pambano hilo ambalo lilikuwa na upinza mkali licha ya kuwa ni mtoto wa kike.

Katika pambano hilo lililopigwa usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, Mwakinyo amemchapa Mcongo kwa pointi kwenye pambano la raundi 12 uzito wa Super Welter kuwania mkanda wa ubingwa wa dunia wa WBF.

Mwakinyo ameendelea kuweka rekodi yake vizuri huku akichafua rekodi ya Mcongo kwani kabla ya kudundwa na mwakinyo alikuwa hajawahi kupigwa katika papmbano lolote.

NA IBRAHIM MUSSA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Leave A Reply