The House of Favourite Newspapers

Ibada ya Misa Kuwaombea Wazazi wa Shigongo Yafanyika Bupandwamhela – Pichaz

Wanakwaya wa Kwaya ya Mt. Maria, Kanisa Katoliki, Kigango cha Bupandwamhela wakiiimba wakati wa ibada hiyo.

FAMILIA ya Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, leo Jumatatu, Desemba 24, 2018 imefanya ibada maalum ya kuwaombea marehemu wazazi wao ambao ni Baba yao Mzee James Bukumbi na mama yao, Bi. Asteria Kapela pamoja na marehemu wengine wa familia hiyo ambao walikwisha fariki dunia.

Padri Faraja Hilali akiendesha ibada hiyo.

Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwao Bupandwamhela, wilayani Sengerema mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na mamia ya  ndugu, jamaa na marafiki ambao waliungana pamoja na familia ya hiyo kwa ajili ya maombi yaliyoendana na kubariki makaburi ya marehemu hao.

Sehemu ya wanafamilia wakiwa kwenye ibada hiyo.

Mzee James Bukumbi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers, James Bukumbi alizaliwa mwaka 1933 na kufariki dunia, Agosti 25, 2012 jijini Dar es Salaam, wakati mkewe, Bi Asteria Kapela, alizaliwa Septemba 16, 1931 katika Kijiji cha Kadashi, Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza na alifariki dunia Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dar es Salaam na wote walizikwa nyumbani hapo Bupandwamhela.

Sehemu ya wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika katika ibada hiyo.

Ibada hiyo ya kumbukumbu iliongozwa na Padri Faraja Hilali ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Mwangika.

Sehemu ya watoto wa marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo.

Katika mafundisho yake wakati wa misa hiyo, Faraja amewaasa waumini kumuweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila siku na kutenda matendo mema huku huku akieleza kuwa lengo la kufanya ibada hiyo maalum siyo tena kuomboleza vifo vya wazazi hao wa Shigongo bali ni kusherehekea vifo vyao kutokana na mambo mema waliyoyafanya enzi za uhai wao hapa duniani.

Aidha, Padri Faraja amewaasa waumini, wanafamilia na jamii yote kuisafisha mioyo yao hasa katika kipindi hiki cha Krismasi ambacho ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kriso, kwa kufanya toba na kumrudia Mungu ili  Yesu azaliwe kwenye mioyo yao na wakiwa safi.

Mwenyezi Mungu azilaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!

(PICHA: DENIS MTIMA/ GPL, BUPANDWAMHELA)

Comments are closed.