The House of Favourite Newspapers

Icardi aaga Inter na dongo

STRAIKA wa Inter Milan, Mauro Icardi ameaga zake kwenda kuichezea Paris Saint-Germain huku akirusha madongo kwa klabu hiyo.

 

Icardi kwa muda mrefu alikuwa akivutana na klabu yake amepata nafasi ya kujiunga na PSG kwa mkopo. PSG ilimsajili Icardi, Jumatatu iliyopita kwa mkopo ambapo kipengele cha mkataba kinaruhusu kununuliwa kwa kitita cha pauni milioni 70.

 

Wakati akiaga katika klabu hiyo aliposti kwenye mtandao wa Instagram, takwimu za kuonyesha mabao aliyofunga. Staa huyo raia wa Argentina aliishukuru klabu hiyo kwa kila jambo mtandaoni.

 

Baada ya kutoa shukrani hizo ndiyo akaweka takwimu zake za kucheza mechi 219, kufunga mabao 124 na kutoa asisti 39.

Inter ilishachoshwa na ukorofi wa Icardi kiasi cha kufikia hatua ya kumvua unahodha na kutakiwa kufanya mazoezi peke yake kutokana na shinikizo lake la kuhama, ambapo kuna wakati aligomea mazoezi

Comments are closed.