Rayvanny , Lulu gumzo

WATU weweee! Ndivyo hali ilivyokuwa mapema wiki hii baada ya kudaiwa Rayvanny na Lulu kuna kitu kinaendelea. Mambo yalikuwa hivi; Rayvanny alitupia picha ya Lulu huko Instagram na kusindikiza na ‘emoji’ ya ua jekundu kisha ‘kumtag’ Lulu na ndipo watu mbalimbali walipoanza kushadadia ishu hiyo na kusema kuna kitu.

Miongoni mwa watu waliochangia mjadala huo ni Mondi ambaye naye aliweka ‘kiemoji’ cha ua hilo bila kusema neno ambapo Wolper naye aliibuka na kuweka kiemoji cha makopakopa machoni. Baada ya Wolper kuweka kiemoji hicho, Mondi alirudi tena na kuandika. “Wolper mbeya wewe.” Hata hivyo, si Rayvanny wala si Lulu aliyejaribu kukanusha ishu hiyo au kuthibitisha kwamba kuna kitu kati yao kinaendelea
Toa comment