The House of Favourite Newspapers

Idadi ya Vijana Waliojitokeza katika Uchaguzi Nchini Kenya Yawa Ndogo

0
Vijana wakiwa katika foleni kufanya uchaguzi nchini Kenya

TUME ya uchaguzi nchini Kenya, yasema idadi ya vijana waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi ni ndogo kulingana na matarajio ya Tume hiyo.

 

Watu wanaotarajiwa kupiga kura nchini Kenya ni Watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, lakini Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa idadi ya vijana imekuwa ndogo kulinganisha na Chaguzi zilizopita.

Raila Odinga naye amepiga kura yake

Idadi ndogo ya wananchi nchini humo kushiriki katika uchaguzi, hasa vijana imesababishwa na wagombea Urais nchini humo ambao ni Raila Odinga pamoja na Ruto, ambao wamekuwa wakitoa Sera zilizozoeleka kwa Wakenya na ambazo hazifanyiwi kazi hata na Serikali iliyopo madarakani

Mgombea Urais nchini Kenya William Ruto amepiga kura yake mapema asubuhi

Matatizo makubwa yanayowakabili Wakenya ni pamoja na tatizo la Rushwa na kutokuwa na usawa miongoni mwa wananchi, matatizo hayo hayafanyiwi kazi hata na Serikali iliyo madarakani vitendo hivyo vinawavunja moyo wananchi hasa vijana kushiriki katika uchaguzi unaoendelea sasa nchini humo.

 

Wanachi wa Kenya wanataka mabadiliko katika bei ya mafuta pamoja na bei ya chakula ambavyo vimekuwa tatizo kubwa.

 

Kwa miaka mingi bei ya Mafuta imekuwa ikipanda kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 60% tokea mwanzoni mwa mwaka huu.

 

Leave A Reply