The House of Favourite Newspapers

Raia wa Nchini Kenya Wanapiga Kura Leo Kumchagua Mrithi wa Uhuru Kenyatta

0
Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na William Ruto wakifurahia jambo kwa pamoja

NCHI ya Kenya leo Agosti 9, 2022 inafanya uchaguzi wake mkuu kutafuta mrithi wa kiti cha Rais atakayechukua nafasi ya anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta.

 

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Nchini Kenya IEBC imesema jumla ya wakenya milioni 22 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchini humo.

 

Tayari vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Raila Odinga Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na William Ruto Makamu wa Rais wa Kenya

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa pamoja na chaguzi wamedai kuwa upinzani mkubwa upo kati ya watu wawili ambao ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Wiliam Ruto (55) pamoja na Mwanasiasa mkongwe Raila Omolo Odinga (77).

 

Odinga ni mwanasiasa mkongwe ambaye ameshawahi kuhudumu katika nafasi ya Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka mitano anaungwa mkono na Rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta, tayari Rais Kenyatta ameshawasili na kupiga kura, William Ruto naye tayari ameshapiga kura yake.

 

 

 

 

Leave A Reply