The House of Favourite Newspapers

Idadi ya Wakimbizi wa Ukraine Yafikia milioni 1.5

0

Mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine yaingia katika siku ya 11 huku idadi ya wakimbizi ikitarajiwa kufikia karibu watu milioni 1.5. Urusi na Ukraine zatupiana lawama kuhusu kukwama makubaliano ya kusitisha mapigano.

Idadi ya wakimbizi wa Ukraine inatarajiwa kufikia watu milioni 1.5 huku Urusi ikiendelea na mashambulizi yake ambayo Jumapili 6.3.2022 yameingia siku ya 11. Serikali ya Ukraine imesisitiza kwa za Magharibi juu kuchukua hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuiongezea Ukraine silaha zaidi na kuiongezea Urusi vikwazo.

Moscow na Kyiv zatupiana lawama juu ya kushindikana kwa mpango wa kusitisha mapigano ambao ungeruhusu raia kuondoka kutoka kwenye miji ya kusini iliyozingirwa na vikosi vya Urusi ya Mariupol na Volnovakha. Raia wa Ukkraine waliofanikiwa kuondoka wameingia katika nchi jirani za Poland, Romania, Slovakia na maeneo mengine.

 

Duru nyingine ya mazungumzo kati ya pande mbili hizo imepangwa kufanyika Jumatatu 07.03.2022.

 

Katika hotuba kwenye runinga mnamo Jumamosi usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alitoa wito kwa watu wake walio kwenye maeneo yanayokaliwa nanajeshi ya Urusi kuendelea kupambana.

 

Amesema ni lazima Waukraine wapambane kuuondoa yake uovu wa Urusi katika miji yao, akitoa ahadi ya ya kulijenga upya taifa lake.

Kushoto: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz. Kulia: Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett

Rais Volodomyr Zelensky amesema siku ya Jumapili amezunguzumza kwa njia ya simu na Rais wa Marekani, Joe Biden na walijadili juu msaada wa fedha pamoja na vikwazo- zaidi dhidi ya Urusi katika kipindi hiki ambacho taifa lake linakabiliwa na ongezeko la mashambilizi.

 

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israeal Naftali Bennett amekutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin kwa lengo la kumpa taarifa ya mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

 

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Hebestreit, amesema Bennett na Scholz wamekubaliana kuwa na mawasiliano ya karibu na kwamba lengo lao kubwa ni kuvimaliza vita vya Ukraine, haraka iwezekanavyo.

Katibu Mkuu wa jumuiya ya NATO Jens Stoltenberg.

Rais wa Urusi Vladmir Putin alionya siku ya Jumamosi kwamba nchi yoyote itakayochukua hatua ya kuifunga anga ya Ukraine itazingatiwa na Moscow kuwa imeingia kwenye mzozo huo.

 

Kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky anazitaka nchi za Magharibi kuunga mkono hatua za kuifunga anga yake ili kuminunga mkono nchi yake inayoshambuliwa na Urusi lakini washirika wake hadi sasa wamepinga hatua hiyo, wakihofia kuwa itazidisha vita na Urusi yenye silaha za nyuklia.

 

Katibu Mkuu wa jumuiya ya NATO Jens Stoltenberg na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wote wametoa kauli hiyo ya kukataa kuchukuliwa hatua za kuifunga anga katika ukanda wa Ukraine licha ya maombi ya mara kwa mara ya Ukraine nchi hiyo ya kutaka kuwekwe marufuku ya ndege kuruka kwenye anga yake.

 

Stoltenberg ameeleza kuwa endapo vita vitaenea hatari itakuwa kubwa zaidi na italeta maafa kwa binadamu. Hata hivyo mawaziri wa nchi za NATO waliokutana mjini Brussels hapo jana Ijumaa wameahidi kuweka vikwazo zaidi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amelaumu uamuzi huo ya jumuiya NATO na kusema kuwa ni sawa na kuipa kibali Urusi iendelee kuishambulia nchi yake.

Vyanzo: RTR/AFP/DPA

Leave A Reply