The House of Favourite Newspapers

Idd Azzan Awasili Sentro Kuitikia Wito wa RC Makonda

DAR ES SALAAM: Aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Idd Azzan ameripoti hivi punde katika Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na mtandao wa dawa za kulevya.
Viongozi wengine waliotakiwa kufika polisi kuhojiwa ni  Askofu Josephat Gwajima na  Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ambao waliripoti jana kisha wakaondolewa na kupelekwa kusikojulikana.
 
Endelea kuwa nasi, tutaendelea kukujuza kila linalojili sentro na kwingineko.

Save

Save

Comments are closed.