The House of Favourite Newspapers

Idris Sultan Alamba Shavu KISS Condom

0
Balozi wa Kiss Kondomu nchini, Idris Sultan akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kondomu mpya ya kiume Kiss jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa DKT International nchini Tanzania, Kevin Hudson.

Mchekeshaji maarufu hapa nchini amelamba shavu la ubalozi katika kondom mpya ya Kiss ambayo ni maalum kwa ajili ya kuzuia virusi vya Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa.

Idris amelamba shavu hilo kwenye uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika maonesho ya ubora wake.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini Dkt. Kevin Hudson amesema “Kondomu mpya iliyozinduliwa ya KISS Condom ina harufu nzuri ya Vanilla na ni kondom bora kwa watu wazima walioridhiana. Inadhihirisha kazi kubwa iliyoidhinioshwa na Wizara ya Afya na Mamlaka ya Dawa Tanzania (Tanzanian Medicines and Drugs Authority) katika kukabiliana na kusambaa kwa maambukizi yatokanayo na kujamiiana na mimba zisizotarajiwa,”Alisema Bw. Kevin Hudson, Mkurugenzi Mkazi wa DKT International nchini Tanzania.

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

Kiss Condom ni nembo ya kimataifa inayozalishwa katika viwanda vilivyothibitishwa na WHO. Kitu ambacho kinampa mtumiaji ubora wa juu.   Kiss Condom zitakuwa zinapatikana madukani katika baadhi ya maduka ya rejareja yaliyochaguliwa kuanzia tarehe 12 September.

Kondomu ni mbinu ya uzazi wa mpango ya kizuizi kwaajili ya kujikinga na kupambana na HIV/Ukimwi na STI’s vile vile ni kizuizi cha mimba zisizotarajiwa ambacho hakiathiri homoni za mwili.  Kwa sasa, kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS za mwaka 2020, – Watu wapatao milioni 1.7 nchini Tanzania wanaishi na HIV.  Takwimu za UNAIDS zinaonyesha kwamba kuna maambukizi mapya 77,000 ya HIV kila mwaka, na takribani vifo 27,000 vinahusiana na maambukizi ya AIDs

 

Kiss Condom ni bidhaa ya nyongeza iliyokuja katika muda muafaka miongoni mwa bidhaa nyingi za DKT International Tanzania. Bidhaa zingine ni kama Fiesta na Bull condoms, Vidonge vya uzazi wa mpango vya dharura vya Trust Daisy. (Trust Daisy emergency contraceptive pills) na Dawa ya uzazi wa Mpango ya Trust Lily.  (Trust Lily oral contraceptive pills).

Leave A Reply