The House of Favourite Newspapers

Idris Sultan Kaanza Mwaka na Dili Jipya Mjini!

                    Mchekeshaji maarufu Bongo, Idris Sultan.

MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Idris Sultan, kupitia akaunti yake ya Insta amepost picha akiwa amevaa  nguo ya ndani ya kampuni ya Calvin Klein na kuonyesha kuwa mwaka huu ni mwaka wa kupiga pesa kwake.

Mwishoni mwa mwaka 2017, kijana huyo amekuwa akiposti picha zikimuonyesha amevaa nguo za ndani za kampuni ya Calvin Klein zinazovaliwa na mastaa kadhaa akiwemo Trey Songz.

Kupitia mtando wa kijamii wa Instagram, Idris amepost picha nyingine na kuandika “I know it’s January but I’m just bad like that, no time to waste. Money monster #MyCalvins #CalvinKlein #PreShoot #2018”

 

Kutokana na posti hiyo huenda Idris amepata shavu jipya katika kampuni hiyo huku akiwa mbioni kushoot filamu mpya ya “The Blue Maurtius” ya nchini Marekani inayosimamiwa na kampuni ya D Street Pictures na Benoraya Pictures.

Comments are closed.