The House of Favourite Newspapers

IGP Sirro, Ole Sabaya Kumtetea Mbowe

0

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamesomewa maelezo ya mashtaka yanayowakabili leo Jumatatu, Agosti 23, 2021 ikiwemo;

 

1. Kula njama za kutenda ugaidi (kulipua vituo vya mafuta)
2. Kutenda ugaidi kwa kusababisha majeraha kwa Ole Sabaya.

3. Mhe. Mbowe alitoa laki 6 kwa ajili ya kufadhili matendo ya Kigaidi.

4. Watuhumiwa wote kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi.

5. Mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi

6. Mshtakiwa wa kwanza akituhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 

Mbali na Mhe. Freeman Mbowe, wanatuhumiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya.

 

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mashahidi 24 na vielelezo 19 akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai, Robert Boaz, watatoa ushahidi kwa upande wa mashtaka.

 

Hayo ameyasema leo, Agosti 23, 2021 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin kuongoza jopo la mawakili wa upande wa mashtaka wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo (Committal Proceedings) washtakiwa hao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

 

Peter Kibatala, wakili wa upande wa utetezi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwamba miongoni mwa mashahidi wao watakuwa, aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na IGP Simon Sirro hivyo ameiomba mahakama kuwaleta mahakamani mashahidi hao.

 

Vielelezo vya kesi hiyo vimefungwa rasmi na kesi imehamishiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo ndiyo ina mamlaka kisheria ya kusikiliza kesi ya ugaidi.

 

Leave A Reply