The House of Favourite Newspapers

Ijue Hoteli ya Kwanza Duniani Iliyopo Angani

 

KITUO cha Aurora ni hoteli ya kwanza duniani – kwenye mzunguko wa orbiti katika anga za juu ambayo ilinuiwa kusisimua safari za duniani

 

Tangazo rasmi kuhusu mpango huo lilitolewa Aprili mwaka jana huko San Jose, California, Marekani. Imejengwa kwa ukubwa wa ndege kubwa ya kibinafsi, itakayoruhusu watalii kupaa maili 200 juu ya ardhi ya dunia, na kupata fursa ya kutupia jicho mandhari ya sayari na mwanga wa kaskazini na kusini.

 

Gharama si nyepesi: safari hiyo ya siku 12 kwenye kituo cha Aurora inayotarajiwa kufanya ziara ya kwanza ya kitalii mwaka 2022, ni  Dola za Marekani mil. 9.5 kwa mtu mmoja.

 

Hata hivyo, kampuni hiyo inasema orodha ya watu wanaosubiri safari hiyo ya kitalii inakusanywa miezi saba kabla ya safari yenyewe.

 

“Sehemu ya hisia tunayotaka kuwapatia watu ni kujua maisha halisi ya mwanaanga za juu yalivyo,” amesema Frank Bunger, muasisi na mkurugenzi mtendaji wa Orion Span, kampuni inayosimamia uidhinishaji wa hoteli hiyo ya Aurora.

 

“Lakini tunatarajia wageni wengi watakuwa wakichungulia nje ya madirisha na kuwaita kila wanaowajua, na iwapo watachoka, tuna tunachokita ‘holodeck,’ mfumo wa uhalisia unaoonyesha hali ilivyo, na unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya. mfano kuelea katika anga za juu, kutembea kwenye mwezi na hata kucheza golfu.”

 

 

Inatarajiwa wageni katika Aurora watajaribu kufanya mambo tofuati katika muda watakaokuwa wakiishi katika hoteli hiyo, kama kujaribu kupanda chakula kama inavyofanywa sasa na moafisa katika ISS.

 

Watu wengi katika taaluma ya sayansi wanaiona kama hatua isiyoepukika katika maisha ya mwanadamu. Lakini kuna msemo wa kale kwamba: jihadhari kabla ya hatari.  Kusema kwamba safari ya raia kwenda katika anga za juu ni kitu kilicho katika kiwango cha msingi, bado haielezi hatua imepigwa kiasi gani.

 

 

Kila mmoja anakubali kwamba utalii katika anga za juu ni jambo kubwa.  Ulianza mnamo 2001 wakati raia wa Marekani Dennis Tito alipolilipa shirika la anga za juu la Urusi Dola mil. 20 ili kuzuru kituo cha ISS kilichopo huko. baadhi ya mataifa tayari yameidhinisha msingi katika sekta hiyo katika siku zijazo.

 

Lakini wataalamu wanasubiri kuona iwapo utalii wa raia katika anga za juu unaweza kutekelezwa na kwa namna gani. Kilichosalia kubainishwa ni usalama, na viwango vya uhandisi kwa mfumo wa usafiri wa raia katika anga za juu.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.