The House of Favourite Newspapers

TFF YAMFUNGIA NINJA WA YANGA – VIDEO

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesikiliza shauri la mchezaji wa Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye alilalamikiwa kwenye kamati hiyo kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union.

 

Ninja alifika mbele ya kamati kujitetea na alikiri kosa kwamba alimpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union baada ya kuoneshwa video za tukio lenyewe lakini alijitetea kwamba hakuwa na kusudi la kufanya hivyo, alikuwa akijaribu kumzuia asipite baada ya kuona amepiga pasi fupi kwa mchezaji mwenzake.

 

Kamati baada ya kupitia ushahidi na utetezi, kamati imemtia hatiani Ninja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu pinzani na kamati imempa adhabu ya kufungiwa michezo mitatu mfululizo lakini hata hivyo, haki ya kukata rufaa kwa mchezaji huyo ipo wazi.

Comments are closed.