The House of Favourite Newspapers

Ile Ishu ya Kina Makame Kutimuliwa Kwenye Nyumba, Ipo Hivi…

0

MAPEMA jana, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ilikuwa ikisambaa picha ikiwaonyesha baadhi ya wachezaji wa Yanga, Abdulaziz Makame, Adeyum Saleh na Ally Ally wakionekana wakihamisha vitu maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Picha hiyo ilizua maswali mengi ambapo wengi walikuwa wakisema wachezaji hao walifukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi maeneo hayo kutokana na kushindwa kulipa kodi, hivyo hawakuwa na pa kwenda.

Spoti Xtra baada ya kuiona picha hiyo pamoja na maelezo hayo, lilizungumza na Makame kupata uthibitisho wa hicho na kuweka mambo sawa.

“Kuhusu picha ni kweli ni sisi jana (juzi Jumanne) tulikuwa tunahama Kariakoo na kuelekea Kinondoni ambapo kuna nyumba mpya tumepata ambayo ni nzuri kushinda tulipokuwa awali.

 

“Watu wanasema eti tumefukuzwa tulipokuwa tunaishi, siyo kweli, tumehama wenyewe baada ya kupata nyumba nzuri zaidi na si kingine,” alisema Makame.

Leave A Reply