The House of Favourite Newspapers

Championi, Spoti Xtra Baba Lao, Ndinga Mpya Kutolewa kwa Wasomaji

0
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (‘TFF), Athuman Nyamlani akikata utepe wa zawadi ya gari aina ya Toyota Funcargo ambayo itatolewa kwa mshindi wa Promosheni ya bahati nasibu ya ‘Baba Lao’, inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

BAHATI nasibu ya Jishindie Gari Mpya iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, imezinduliwa rasmi leo Alhamisi, Februari 27, 2020.

 

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akimwakilisha rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia.

 

Baadhi ya viongozi wa Global Publishers  wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani (katikati), wakiwa wameshika gazeti la Spoti Xtra na vipeperushi baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa promosheni ya bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na Magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

Bahati nasibu hiyo iliyozinduliwa rasmi leo Alhamisi katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar, mshindi mmoja ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo mpya kabisa.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Nyamlani ameanza kwa kuyapongeza magazeti ya Championi na Spoti Xtra kwa kuandika habari za ukweli na za uhakika, huku akichagiza kwamba yeye ni msomaji mkubwa wa magazeti hayo, huku akiwataka wasomaji wengine kutumia fursa hiyo kujishindia.

 

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ‘Jembe’ akimuonyesha Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani Gazeti la Spoti Xtra ambalo hutoka kila Alhamisi na Jumapili. Kulia ni Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula

 

Nyamlani aliongeza kuwa, ni jambo zuri sana kuona magazeti hayo yanakumbuka wasomaji wake na kurudisha kwa jamii, kwani kuandaa bahati nasibu hiyo ni zaidi ya kutambua mchango wa wananchi ambao siku zote wamekuwa wakisoma magazeti hayo na kupata taarifa mbalimbali za kimichezo.

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akitoa maelekezo kwa wanahabari na wasomaji kwa ujumla, namna ya kushiriki bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na Magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

Mbali na hilo, Nyamlani alipongeza juhudi za waandishi wa Gazeti la Championi na Spoti Xtra, kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi mkubwa bila kumgandamiza yeyote, jambo ambalo limekuwa msaada katika harakati za kukuza michezo hapa nchini.

 

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ‘Jembe’ akitoa maelekezo namna ya kushiriki bahati nasibu ya Baba Lao kupitia Magazeti ya michezo ya Spoti Xtra na Championi.

 

“Mimi ni msomaji mzuri sana wa magazeti haya, ni magazeti mazuri sana ambayo huwa yanaandika habari za ukweli na uhakika, jambo ambalo ni msaada katika maendeleo ya soka letu na michezo kwa jumla, hivyo niwapongeze waandishi na uongozi kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana na sisi TFF.

 

Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani akizungumzia furaha yake  kutokana na uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Saleh Ally na kulia ni Meneja wa Global Publishers Abdallah Mrisho

 

“Kuhusu bahati nasibu, niwapongeze, naamini mnarudisha shukrani zenu kwa jamii ambayo siku zote imekuwa ikiwasapoti katika habari ambazo mnaziandika na wao wananunua magazeti na kuzisoma,” alisema Nyamlani.

 

Kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo, Nyamlani alipata fursa ya kutembelea idara mbalimbali na kushuhudia namna shughuli zinazofanywa na Global Publishers.

 

Hili ni gari aina ya Toyota Funcargo ambalo ndio zawadi ya mshindi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mhariri Mtendaji, Saleh Ally na Mhariri Kiongozi Magazeti Pendwa, Richard Manyota, walimuongoza Nyamlani kutembelea idara tofauti ikiwemo vyumba vya habari vya Championi, Spoti Xtra na Magazeti Pendwa, kitengo cha wasanifu kurasa na IT.

 

Pia Studio za Global TV Online na +255 Global Radio, kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mikutano ambapo ndipo uzinduzi ulifanyika mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti.

 

Mgeni rasmi wa uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao, Athumani Nyamlani (kushoto) akiwasili rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa shindano hilo akiambatana na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, nyuma yao ni Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Saleh Ally, kwa pamoja wakilakiwa na wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group waliokuwepo kushiriki uzinduzi huo.

 

Akizunumzia bahati nasibu hiyo, Meneja Mrisho, alisema: “Tunahitaji wasomaji wetu waweze kujikwamua kiuchumi, ndiyo maana tumetoa zawadi ya gari ambalo naamini kama mshindi atashinda gari hili ataweza kulitumia kama taksi ama usafiri wake binafsi, hivyo watu wanunue zaidi Gazeti la Championi na Spoti Xtra waweze kujishindia.

 

“Gazeti la Spoti Xtra ambalo linatoka kila Alhamisi na Jumapili, linauzwa Sh 500 na Championi linalotoka Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi linapatikana kwa Sh 800 tu.”

 

Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Funcargo ambalo ndio zawadi ya bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

Kwa upande wa Mhariri Mtendaji, Saleh Ally, alisema: “Championi na Spoti Xtra ndiyo magazeti pekee yenye habari bora zilizojaa takwimu na habari za uhakika hapa nchini, hakuna gazeti ambalo utapata kila kitu isipokuwa Championi na Spoti Xtra.

 

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahtisha nchini, Rasul Masoud (kulia) akiwa na Mhartiri wa Gazeti la Championi Jumatano, Philip Nkini wakifuatilia uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

“Lakini pia katika kila shindano au promosheni inayoletwa na magazeti haya, hutoa zawadi za ukweli kabisa tofauti na watu wengine ambao hudanganya, hivyo wasomaji kupitia magazeti haya washiriki na waone jinsi gani watakavyoshinda zawadi kemkem.”

 

 

Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani baada ya uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

Mbali na mshindi kuondoka na gari, pia kuna zawadi zingine zitakazotoka kila wiki ambazo ni simu za mkononi aina ya Smati Kitochi.

 

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

Timu ya Masoko na Usambazaji ya Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

Mkuu wa Idara ya IT wa Global Publishers, Edwin Lindege na Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Lucy Mgina wakiwa kwenye vibe baada ya uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani akizungumza na wanahabari baada ya uzinduzi wa bahati nasibu ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply