IMEFUNUKA WASTARA ALIPENDA KUVUA SAMAKI, KWENDA PORINI

IMEFUNUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii wa filamu za Kibongo, Wastara Juma kufunua siri yake kwamba alipokuwa mdogo alikuwa na tabia ya kuwakusanya watoto wa watu mtaani kwao na kuwapeleka mtoni kuvua samaki.

Akiongea na Ijumaa Wikienda, Wastara alisema enzi hizo alipenda sana kucheza kwenye mito na mara nyingi alikuwa akiwashawishi watoto wa mtaani kwao, huko Morogoro kwenda kuogelea na kuvua samaki, kitendo kilichokuwa kinawakera sana wazazi wa watoto hao.

“Ukweli niliwasum¬bua sana wazazi hasa wa watoto wengine kwani wapo ambao walikuwa hawap¬endi watoto wao kuvuka eneo la nyumbani lakini mimi nilikuwa nikiwashawishi tunakwenda mtoni na tuna¬vua samaki wakubwa na wadogo,” alisema Wastara.

Aidha alisema kuwa, pia alikuwa ni binti aliyependa kwenda sehemu zenye mapori kuangalia ngedere na alikuwa yuko tayari kuwapa chochote kaka zake ili wampeleke huko.
Stori: Mwandishi Wetu

Toa comment