The House of Favourite Newspapers

INASIKITISHA SANA… DENTI APATA JANGA ZITO!

AMA kweli hujafa hujaumbika! Mtoto Sharifa Habibu (16) mkazi wa Kihonda Manyuki Mkoani Morogoro ambaye ni denti wa kidato cha pili, yuko kwenye kipindi cha mateso kwa muda mrefu baada ya mguu wake wa kulia kupata kidonda kisichopona.

Akizungumza na Gazeti la Uwazi, baba wa mtoto huyo, Habibu Habibu alisema binti yake huyo alianza kama mzaha tu kwani siku hiyo alikuwa ametoka kisimani na kwa bahati mbaya walikutana na mwendawazimu wakawa wanakimbia, kwa bahati mbaya alianguka lakini aliinuka na kuendelea kukimbia. “Alivyorudi nyumbani akaanza kuelezea jinsi alivyoanguka,

tukampa dawa ya kutuliza maumivu lakini kesho yake akawa analalamika sana kuwa anasikia maumivu, tukampeleka Hospitali ya Mkuyuni, walimpa dawa lakini akawa halali kabisa kutokana na maumivu,” alisema baba huyo na kuongeza:

“Ilibidi tumrudishe tena hospitali ya mkoa ya Morogoro, kwa kuwa mguu ulishaanza kuvimba, wakamchoma sindano kwenye ule uvimbe. “Baada ya sindano hizo walimfanyia upasuaji na kumtoa usaha kisha walituruhusu lakini kidonda hakikufunga kabisa, yaani toka mwaka 2016 mpaka leo kipo hivyo hivyo.”

Akasema kuwa, kutokana na hali ilivyokuwa mbaya walitakiwa kwenda Hospitali ya Muhimbili lakini walishindwa kwa sababu ya kukosa fedha. “Tunachokifanya ni kumpa dawa tu za kupunguza maumivu, lakini tatizo limekuwa kubwa, mguu huo ushakuwa mfupi kabisa na mwingine umepooza kwa sababu ya sindano. Kingine hatari zaidi akitembea vifupa vinatoka nje na kudondoka,” alisema baba huyo

Aliongeza kuwa, wakati mwingine inabidi kumbeba ili kumpeleka shule kwani uwezo wa kutumia pilipiki haupo na magongo akiyatumia maumivu yanazidi. Mtanzania mwenzangu uliyeguswa na tatizo la mtoto huyu unaweza kusaidia chochote kupitia namba 0787 511 298.

Comments are closed.