The House of Favourite Newspapers

INATISHA! MJAMZITO Ajipasua TUMBO Ajizalishe, RPC Asimulia! – Video

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Joyce Kalinda anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo.

 

Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua tumbo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Dkt. Hashi Mvogogo, amesema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo.

 

“Mwanamke huyo alifika katika Kituo cha Afya cha Kirando Alhamisi iliyopita saa tisa alfajiri na kuanza kupiga kelele, akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua. Kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo kusubiri kidogo kisha alikwenda kumhudumia mgonjawa mwingine, lakini aliporejea mahali apokuwepo hakumkuta.

 

“Alfajiri saa 11, mjamzito huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamembeba mtoto mchanga. Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaji mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.”

INATISHA! Mama MJAMZITO Ajipasua TUMBO Ajizalishe, RPC Asimulia!

Comments are closed.