The House of Favourite Newspapers

Infinix na Tigo Wazindua Mkombozi wa Wengi “Infinix Smart 6 na Hot 12i”

0

DAR ES SALAAM. Tarehe 5 Aprili, 2022. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali Tanzania, Tigo Tanzania, imeshirikiana na INFINIX Tanzania kuzindua simu za gharama nafuu INFINIX SMART 6 shilling.220,000 na HOT 12i.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema kuwa “Tunafuraha kuzindua rasmi simu pendwa Infinix HOT 12i na Infinix Smart 6. Infinix HOT 12i ni simu mahiri mpya ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kama zilivyo simu zetu siku zote, Infinix ina RAM ya kutosha, teknolojia ya fusion huruhusu simu za HOT 12i kuongeza RAM Mfano 3GB ya RAM inaweza kuongezwa mpaka kuwa 6GB ya Ram, Screen kubwa ya 6.6HD+” 90Hz Pro-Level ya elektroniki itakayokufanya ufurahie kucheza Game katika simu yako.

Pia Inakuja na betri ya 5000mAh, Chipset Helio, itakayokufanya utumie simu yako katika masuala mbalimbali kama kucheza game, kuingia kwenye mitandao ya kijamii na mambo mengine mengi bila kuhofia chaji kuisha”.

 

“Tumejitolea daima kubuni simu mahiri zenye utendakazi bora na za kisasa kwa wateja wetu kwa gharama nafuu kila wakati. Infinix HOT 12i na Smart 6 zimepata mafanikio katika utendakazi ulioboreshwa, ustahimilivu wa muda mrefu, muundo wa kisasa wa Smart 6 ukihakikisha ulinzi thabiti kwa kumkinga mtumiaji dhidi ya bacteria ambazo zinaishi nje/juu ya simu zetu kutokana na pirikapirika mbalimbali”, alisisitiza Aisha Karupa.


Mtaalam wa Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Blass Abdon amesema kuwa  “Tunafuraha tena kuungana na INFINIX Tanzania kuzindua simu mpya za kisasa ambazo zitaimarisha zaidi lengo letu la kuunganisha watanzania katika mfumo wa huduma za Kidigitali kote nchini. Na Mfumo huu unaimarisha zaidi imani ya washirika wetu hasa katika mtandao wetu wa 4G uliosambaa kote nchini”.

 

“Kulingana na mkakati wetu wa kuharakisha kupenya kwa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB 78 za intaneti BURE kwa muda wa mwaka mmoja kwa wateja wote watakaonunua simu janja za Infinix Smart 6 na HOT 12i”

 

“Tunawakaribisha wateja Wetu wote katika maduka ya Infinix na Tigo Nchini kujipatia simu hizi mpya na za kisasa na kufurahia maisha ya Kidigitali ” Alimalizia Abdon.

 

 

Leave A Reply