The House of Favourite Newspapers

INFINIX Yaja na Toleo Jipya – Ininix Hot 10

0
Afisa Uhusiano wa Infinix Tanzania, Aisha Karupa akizungumza na wanahabari.

Kampuni ya uzalishaji wa simu za mkononi ya Infinix, imetangaza uwepo wa toleo jipya katika matoleo ya HOT. Infinix HOT 10 iliingia rasmi mwanzoni mwa wiki hii katika maduka ya simu nchini Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya simu zote zenye thamani ya Sh.300,000 hadi Sh.350,000.

Ni simu iliyotokea kupendwa na vijana zaidi na hii ni kwa sababu imebeba sifa zifuatazo kama vile;

Processor aina ya MediaTek Helio G70, battery yenye ujazo wa 5200mAh, kamera zenye megapixel 16+2+2+QVGA kwa megapixel 8 selfie, memory yenye GB 64+GB 3RAM, kioo cha nchi 6.78 nateknolojia ya DTS Audio.

Infinix HOT 10 ni simu yenye kuwalenga vijana wa kisasa wenye  kupenda kwenda na wakati lakini pia ni  simu ya kwanza katika  matoleo ya HOT Series kuwa na processor yenye kasi aina ya MediaTek Helio G70 na teknolojia ya MediaTek Hyper Engine. MediaTek HyperEngine ina kazi nyingi katika    uchezaji games na kazi mojawapo ni kubeba na kuendesha games zenye ujazo mkubwa  pasipo kuzidiwa mzigo.

Kioo cha Infinix HOT 10 chenye Inch 6.78 humsaidia mtumiaji ku   weka application zake katika mpangilio mzuri na kuziona katika hali ya ukubwa zaidi. Infinix HOT 10 haina mvuto katika upande wa kioo tu lakini hata umbo lake lina wembamba wa mm9, hivyo unaweza kuihifadhi hata katika mfuko wa surual au shirt pasipo kuharibu show ya muonekano wako.

Teknolojiaya AI yenye megapixel 8 za selfie na megapixel 16 zinapiga picha zenye uhalisia pasipo kujali nyakati wala  mazingira, kamera hizi mbili zinateknolojia ya AI smart beautification na super night view mode kwajili ya ung’arishaji picha katika nyakati  zote.

“Battery ya HOT 10 yenye ujazo wa mAh 5200 inadumu na chaji kwa kipindi cha muda mrefu hata pasipo kuzima data ya simu yako na huku ukiendelea  kucheza gemu na kujiburudisha na mziki   mzuri unaochujwa kwa kutumia teknlojiaya DTS Audio”alisema Afisa wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Aisha Karupa.

Leave A Reply