The House of Favourite Newspapers

Infinix Yawapa Fursa Wateja wa Note 40 Series Kwenda Dubai, China na Mkwanja wa Hadi Mil. 2

0

 

 

Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix @infinixmobiletz  imewatangaza washindi wa Promosheni ya Paa na Manoti wa wiki ya kwanza tangu kuanza kwa promosheni hiyo ambapo ticket ya kwanza ya usafiri wa ndege imemdondokea Sindayihaririza Hilaire ambaye amejishindia baada ya kununua simu aina ya Infinix NOTE 40 pro katika moja ya maduka ya simu Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Infinix wameeleza kuwa promosheni hiyo iliyoanza April 15, 2024 bado inaendelea mpaka April 30, 2024 ambapo katika kipindi hiki chote cha promosheni, ukinunua simu za Infinix moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye fursa ya kujishindia tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi kwa nchi kama Dubai, China pamoja na safari za ndani.

“Nafasi ndiyo hii ya Kupaa na Manoti mpaka Dubai, China na safari za ndani, unachotakiwa kufanya ni kujipatia NOTE 40 au NOTE 40 Pro kwa bei ya punguzo ambapo mbali na kujishindia tiketi ya ndege, pia utajishindia kitita cha shillingi 2,000,000, Laptop, smart watch, earpods na zawadi nyingine kibao,” imeeleza taarifa kutoka Infinix.

Infinix pia imetoa punguzo kubwa la bei kwa simu zao mpya za toleo la NOTE 40 na NOTE 40 Pro ambazo zinafanya vyema sokoni kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kupitisha chaji kwa haraka ambapo kwa sasa NOTE 40 pro inauzwa shillingi 633,000 kutoka Shillingi 680,000 ya awali na NOTE 40 Pro inauzwa Shillingi 790,000 kutoka shillingi 850,000 ya awali.
NOTE 40 Pro ina fast charge ya Watt 70 na Magnetic Wireless ya Watt 20 ambapo kwa dakika 16 tu simu inakuwa imefikisha asilimia 50 ya chaji ambapo ni simu pekee yenye sifa hii na yenye gharama nafuu katika simu za daraja lake.

 

Kwa taarifa zaidi piga simu namba 0656317737 au tembelea akaunti za mitandao ya kijamii za Infinix @infinixmobiletz.

Leave A Reply