The House of Favourite Newspapers

Injinia Hersi Atoa Kauli ya Kibabe Aahidi Ubingwa Wa 30 Yanga

0
Injinia Hersi Said

UNAAMBIWA baada ya Yanga SC, kutwaa ubingwa wa 29 ndani ya Ligi Kuu Bara, tayari rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said ametoa kauli ya kibabe kwa kusema usajili watakaoufanya msimu ujao, lazima watabeba tena kombe hilo.

Jana Yanga ilifanya sherehe za ubingwa wake huo wa 29 baada ya kukabidhiwa rasmi kombe lao juzi Ijumaa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons ambao Yanga ilishinda 0-2 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Akizungumza na Spoti Xtra, Hersi alisema pamoja na kuwa wametwaa kombe hilo mara mbili mfululizo, bado watajipanga kuhakikisha msimu ujao wanabeba tena na kufanya klabu hiyo kufikisha ubingwa wa 30 katika historia yao.

“Msimu ujao tutaongeza ubora kwenye kikosi chetu, nikuhakikishie kuwa katika mabadiliko na uboreshaji wa kikosi tutakaoufanya kwenye dirisha lijalo la usajili, ni wazi kabisa tutafika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mbali na hivyo, nikuhakikishie tu kuwa mwakani tutarudi na kuchukua ubingwa kwa mara ya tatu, hilo sina wasiwasiwa nalo kwani tutajipanga na tutafikia malengo na dhamira yetu ya kufikisha ubingwa wa 30,” alisema Hersi.

STORI NA MUSA MATEJA

Leave A Reply