The House of Favourite Newspapers

Inonga Ampa Jeuri Benchikha Simba dhidi ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast

0
Beki wake wa kati Mkongomani, Hennock Inonga

KUREJEA kwa beki wake wa kati Mkongomani, Hennock Inonga kumempa jeuri Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhaki Benchikha ya kupata matokeo mazuri watakaporudiana dhidi ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

Beki huyo alirejea nchini juzi akitokea Ivory Coast, ambako alikuwa na timu ya taifa ya DR Congo iliyokuwa inacheza Kombe la Mataifa Afrika kabla ya kutolewa hatua ya Nusu Fainali.

Nyota ni kati ya wachezaji tegemeo waliokuwa wanaunda kikosi cha kwanza cha timu hiyo, na kufika hatua hiyo ya nusu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Benchikha alisema kurejea kwa beki huyo, kumeimarisha kikosi chake katika nafasi ya ulinzi ambayo awalikuwa ikichezwa na Kennedy Juma na Hussin Kazi waliokuwa wakibadilishana.

“Maandalizi yamekanilika kwa kiasi kikubwa kuelekea mchezo huo, ninafurahia kuona morali ya kila mchezaji ikiwa kubwa kabla ya kukutana dhidi ya Asec Mimosas Jumamosi hii.

“Nina matumaini makubwa ya timu yangu kupata matokeo mazuri, baada ya kurejea kwa beki wangu Inonga aliyekosekana katika michezo kadhaa ya ligi.

“Ninafahamu umuhimu wa mchezo huu, ambao lazima tupate ushindi ili tufuzu hatua inayofuatia, naheshimu ubora wa Asec Mimosas ambao tayari wamefuzu Robo Fainali, lakini tutahakikisha tunapambana kupata matoke mazuri,” alisema Benchikha.

ALI KAMWE AWAVAA SIMBA TABIA ya KUOMBA MECHI ISOGEZWE MBELE – ATANGAZA BALAA JUMAMOSI…

Leave A Reply