The House of Favourite Newspapers

Instagram yaongeza urefu wa kupost video

0

Instagram-Explore

Watumiaji wa Instagram sasa wanaweza kupost video zenye urefu wa sekunde 60 kutoka sekunde 15 za awali.

Mabadiliko hayo yamefanyika kuanzia Jumanne hii kwenye app hiyo ya iOS na Android na yataanza kupatikana kwa watumiaji wote duniani .

Video zimekuwa muhimu kwenye app hiyo yenye watumiaji milioni 400 duniani. Uwezo wa kuweka video ndefu, kutawafanya watumiaji kutumia muda mrefu kwenye app.

Tayari Diamond aliyepo ziarani Ulaya ni miongoni mwa watu walioanza kufaidi huduma hiyo.

“From 15 seconds to 1minute!!!..Mwe! Asante Insta kwa kutuongezea urefu wa hizi clip tujinafasi,” ameandika kwenye video aliyoiweka.

From 15 seconds to 1minute!!!..Mwe! Asante Insta kwa kutuongezea urefu wa hizi clip tujinafasi!😃

A video posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Leave A Reply