The House of Favourite Newspapers

Instincts Records Yazinduliwa Na ‘Falling In Love’

Meneja wa Shose, Joseph Mwanukuzi (kushoto) akimtambulisha kwa mashabiki zake.

LEBO mpya ya muziki wa ya Instincts Records iliyopo Kinondoni-Studio jijini Dar jana imefanya uzinduzi wa lebo hiyo itakayosimamia kazi za wasanii wa Kibongo kwa levo za kimataifa na kuzindua video ya ‘Falling in Love’ ya msanii Shose Modest ‘Shose’ ambaye ameanza kusimamiwa na kampuni hiyo.

Shose Modest ’Shose’ akihojiwa na wanahabari wakati wa hafla hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo wadau na wasanii mbalimbali walihudhuria kushuhudia uzinduzi huo, ulioambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

 

Meneja wa Shose, Joseph Mwanukuzi, akizungumza jambo na wanahabari.
Shose akiimba.
.Mtayarishaji wa muziki Abbah akizungumza jambo.


Baadhi ya warembo wakifuatilia kwa makini nyimbo iliyokuwa ikiimbwa stejini na Shose.
Msanii Izzo B akiwa na Bella kwenye uzinduzi huo

Shose akipozi katika ‘red carpet’.
Mashabiki wakiburudika katika hafla hiyo.

Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi wa Lebo ya Instincts Records, Joseph Mwanukuzi,  alisema kuwa wamejipanga kufanya mabadiliko ya kuwasimamia vizuri wasanii na kuwafanya wanufaike na kazi zao.

“Lengo letu ni mabadiliko ya sanaa nchini, wasanii wanufaike kama ilivyo kwa wasanii wa mataifa mengine, kwa kuanza tunamsimamia Shose, na kila mwaka tutakuwa tunawasaini wasanii wanne, ambao wana nidhamu ya kazi, wanajituma na wana kipaji, hivyo ndiyo vigezo vyetu,” alisema Mwanukuzi.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria katika uzinduzi wa lebo hiyo ni Country Boy, Izzo B, Bella, Mchizi Mox, One Incredible na wengineo.

 

PICHA STORI: DENIS MTIMA NA GABRIEL NG’OSHA/GPL

Comments are closed.