The House of Favourite Newspapers

Iran Yazuia WhatsApp, Instagram Huku Maandamano ya Mahsa Amini Yakiongezeka

0
mtandao wa Watsup na Instagram

IRAN imezuia upatikanaji wa mitandao ya kijamii ya Instagram na WhatsApp huku kukiwa na maandamano ya kupinga kifo cha mwanamke aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa mujibu wa wakaazi na shirika la NetBlocks.

 

Kukatika kwa mtandao kwa kiasi kikubwa pia kuliripotiwa kote nchini huku kampuni moja kubwa ya simu za rununu ikiwa imetatizwa na kuwaacha mamilioni ya Wairani nje ya mtandao.

Maandamano Iran

Kifo cha wiki iliyopita cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22, ambaye alikamatwa na polisi wa maadili mjini Tehran kwa mavazi yasiyofaa kimeibua wimbi la hasira juu ya masuala ikiwa ni pamoja na uhuru katika Jamhuri ya Kiislamu na uchumi unaoyumba kutokana na vikwazo.

 

Takriban waandamanaji sita sasa wameuawa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran na maafisa, pamoja na afisa wa polisi na mwanachama wa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali. Hata hivyo makundi ya wanaharakati yanasema idadi ya vifo ni kubwa zaidi.

 

Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply