The House of Favourite Newspapers

Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Waendelea Kuandamana Kupinga Kurudi kazini Nchini Nigeria

0
Maandamano

WALIMU wa vyuo vikuu wanaogoma nchini Nigeria wamesema watakata rufaa dhidi ya agizo la mahakama ya usuluhishi inayowataka kusitisha mgomo wao wa miezi saba na kurejea kazini.

 

Mahakama ya Kitaifa ya Viwanda ilitoa agizo hilo Jumatano wakati ikizingatia kesi ya serikali kupinga mgomo huo.

 

Lakini Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu ulisema wanasheria wake tayari walikuwa wanawasilisha rufaa na kuwataka wanachama wake kuwa watulivu.

 

Serikali ilifika mahakamani kuwazuia wahadhiri hao kuendelea na mgomo wao, baada ya pande zote mbili kushindwa kutatua tofauti zao. Ilisema mgomo huo utasababisha uharibifu usioweza kurekebishwa kwa wanafunzi wa Nigeria na kwa nchi ikiwa hautasitishwa.

 

Kwa muda wa miezi saba iliyopita, wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma wamesimamisha masomo kote nchini kutokana na kutoelewana na serikali.

 

Wahadhiri hao waliishutumu serikali kwa kukosa kutimiza baadhi ya makubaliano yaliyoafikiwa na muungano huo miaka 10 iliyopita.

 

Chama cha wanafunzi hata hivyo kiliitaka serikali kutoona uamuzi huo kama ushindi dhidi ya wahadhiri hao.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

 

 

 

Leave A Reply