The House of Favourite Newspapers

Irene Uwoya Afunguka Sababu ya Kutozeeka Akionekana Msichana Mrembo

0
Irene Pancras Uwoya

 

Irene Pancras Uwoya; ni staa nembo wa Bongo Movies na ni mwanamama mjasiraiamali maarufu nchini Tanzania ambaye ametoa siri ya kutozeeka kwake na kuzidi kuonekana kabinti kabichi, IJUMAA lina exclusive.

Kumekuwa na mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii juu ya uzuri wa Uwoya mwenye umri wa miaka 33, akielezwa kuwa baadhi ya watu hukataa kwamba ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, Krish Ndikumana.

Hii ni kutokana na kuendelea kuwa ‘kinanda’ zaidi kila kukicha.

 

KAMA JLO NA KIM

Wengine wanasema kuwa, huwenda Uwoya anatumia dozi ya kutozeeka kama akina Jeniffer Lopez (JLO) na Kim Kardshian wa Marekani.

Wengine wanadai kuwa huwenda Uwoya amefanya sajari ya ngozi ili kuonekana ya mtoto huku wengine wakidai kwamba, ni kwa sababu anaogea maziwa ya ng’ombe!

Wengine wanasema kuwa, Uwoya ni muigizaji ambaye watu wanatamani kumuangalia kuliko kuliko hata filamu yenyewe anayoigiza.

UKIKUTANA NAYE LAIVU SASA

Wengine wanasema kuwa, Uwoya anavutia kumtazama runingani, lakini ukikutana naye ‘laivu’ utaamini kuwa kamera zina chuki naye, kwani ni mzuri maradufu ya yule unayemuna runingani.

Sasa; mbali na runingani, Uwoya ni habari nyingine kwenye mitandaoni mitandao ya kijamii.

 

Uwoya akipsoti picha mpya, hadi wasanii wenzake na watu wake wa karibu akiwemo Aristote na Shamsa Ford, wanavutiwa naye na kummwagia sifa kedekede.

 

Wapo wanaosema kuwa, filamu inaweza kuwa mbaya, lakini wakijua Uwoya yumo ndani, basi watajilazimisha kuitazama ilimradi tu wamuone na siyo kujua stori ya filamu husika.

 

Hata hivyo, wapo wanaosema Uwoya anavutia wanaume wakware na si kweli kwamba ni mzuri kiivyo.

 

Wanaobeba hoja hiyo wanasema kuwa, wanawake walio wengi wanapovaa nguo za nusu utupu wanaonekana wazuri au wenye mvuto kwa wanaume wenye matamanio, akiwa amevaa kama mwanamke kamili, huwezi hata kumtamani.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, ukubwa wa jina na ubora wa sura, umbile na rangi yake, havina uhusiano wenye tija na tabia zake za binafsi na kwamba ni vitu viwili tofauti.

 

SABABU KUTOZEEKA

Staa huyo mwenye pesa zake anasema sababu ya yeye kutozeeka huku kila siku akionekana msichana mdogo, tena mrembo, cha kwanza ni kuweza kuziweka stresi za maisha pembeni.

 

Uwoya anasema kuwa, pamoja na kuweka msongo wa mawazo kando, ila yeye ni mwanamke ambaye anajipenda kupitiliza na kujua thamani yake halisi na kutoyumbishwa  na mtu yeyote kisha anajipenda yeye kwanza na nafsi yake.

 

“Mimi najipenda sana na ni mwanamke ninayejijali mno. Pia siupi muda kabisa ubongo wangu ufungamane na kitu chochote hasi kwenye maisha yangu.

 

“Lakini kubwa kuliko ni kwamba mimi najipenda kwanza, halafu mwingine atafuata, nafsi yangu ni ya kwanza kwangu,” anasema Uwoya akimshukuru pia Mwenyezi Mungu kwa kumuumba na udongo mzuri.

Stori; Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply