Isaya Mwita wa Chadema ndiye Meya wa Dar
Meya Mteule wa jiji la Dar es salaam Issaya Mwita Chalres kutoka kata ya vijimbwweni (UKAWA)
Fomu ya uthibitisho wa matokeo ya uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam.
Taswira ya ukumbi ilivyokuwa
Aliyekuwa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema,Edward Ngoyayi Lowasa (katikati mwenye sharti jeupe) akiwa katika hafla iyo
Baadhi ya viongozi wa chadema wakiwa wanafuatilia uchaguzi uliokua ukiendelea
Kura zikihesabiwa ukumbini hapo
Ilivyooneka nje ya ukumbi wa karimjee
Ulinzi ulivyokuwa umeimalishwa nje ya ukumbi
Picha zikionyesha taswila mbalimbali ya uchaguzi huo wa Meya wa jiji la Dar es salaam.
Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo ameibuka mshindi katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam kwa kura 84 huku Omari Yenga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kura 67 na kura 7 zimeharibika.
Wajumbe 158 ndiyo walipiga kura katika uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjeee jijini Dar es Salaam.
(Na Denis Mtima na Chande Abdallah/Gpl)
Comments are closed.