The House of Favourite Newspapers

ISHA MASHAUZI ALIVYOSHEREHEKEA BETHDEI NA WANAFUNZI

Muimbaji wa taarab na Mkurugenzi wa Kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhani Makongo maarufu kama Isha Mashauzi akikata keki huku akiimbiwa “kata keki tuuule”.

Muimbaji wa taarab na Mkurugenzi wa Kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhani Makongo maarufu kama Isha Mashauzi leo amesherehekea siku yake ya kuzaliwa na wanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi Mmoja ambayo alisoma.

Akiwalisha wanafunzi.

Katika sherehe hiyo Isha aliongea na wanafunzi hao kisha akalishana nao keki kama ilivyo kawaida.

Akimlisha keki mmoja wa walimu kwa niaba ya wenzake.

Baada ya hafla hiyo Isha amesema ameamua kuifanyia bethdei hiyo shule hapo kutokana na maarifa mengi aliyoyapata akiwa mwanafunzi wa shule hiyo aliyosoma kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

Paparazi wetu Richard Bukos naye alikula keki ili kuihakiki ubora wake.
Akiwapa juisi wanafunzi hao.
…Akiongea jambo na wanafunzi hao.
Akiwa nao katika picha ya pamoja.

PICHA/HABARI: RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.