The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Fiston Mayele na Yanga Ipo Hivi… Akutana na Viongozi

0
Mkongomani, Fiston Mayele.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele amefikia sehemu nzuri ya mazungumzo yake na Yanga kuhusiana na mkataba wake mpya.

Awali ilielezwa kuwa, Mayele ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Yanga amepata ofa nzuri kutoka klabu za Uarabuni ikiwemo Pyramids na zingine za Qatar na hapa Bongo hivyo aliuomba uongozi asepe kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Juzi Jumatatu, Mayele na uongozi wa Yanga walikuwa na kikao cha mwisho kujadiliana kuhusu ishu hiyo ambapo upande wa Yanga walikuwa wakipambana kumshawishi abaki huku yeye akitoa ofa yake ya mshahara wa Sh 40Mil ili aongeze mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinasema mabosi wa timu hiyo, wamekubali kumpatia ili aendelee kubakia hapo katika msimu ujao huku dau lake likifichwa.

Imeelezwa kuwa Yanga wamekubali kumlipa mshahara huo ili abakie hapo katika msimu ujao, akiingia katika rekodi kubwa ya kuwa mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi hicho cha fedha katika Ligi Kuu Bara.

Awali Yanga waliweka ofa ya mshahara wa Sh 28Mil ili abakie Jangwani kwa misimu miwili zaidi lakini Mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu Bara alikataa.

Mmoja wa Viongozi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa dili hilo limekamilika kwa asilimia kubwa na mshambuliaji huyo ataendelea kubakia hapo kwa mshahara huo wa Sh 40Mil.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi wa usajili alisema kuwa mshahara huo mpya ataanza kulipwa mara baada ya msimu wa 2023-24 kumalizika.

Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo ataanza kuchukua mshahara wa Sh 16Mil kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja na baada ya hapo atachukua huo mpya wa 40Mil msimu wa 2024-25.

“Kwa kifupi uongozi wa Yanga wamefanikiwa kumbakisha Mayele, baada ya malumbano ya muda mrefu kati yake na uongozi baada ya yeye kuomba aboreshewe baadhi ya mahitaji yake katika mkataba wake mpya.

“Kitu cha kwanza alichoomba aboreshewe ni mshahara kwanza akiomba apatiwe Sh 40Mil katika mkataba wake mpya, mazungumzo yalikwenda vizuri juzi na kufikia muafaka mzuri wa yeye kukubali kubakia hadi 2026.

“Makubaliano yamekamilika kati ya Yanga na Mayele kwa kwa mkataba wa miaka miwili hadi 2025 ataendelea kusalia Yanga akimalizia mkataba wake wa mwaka mmoja,” alisema mtoa taarifa huyo.

Yanga kupitia Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said juzi alisema kuwa: “Hatutamuachia mchezaji yeyote katika msimu huu aliyekuwa katika mipango ya timu kuelekea msimu ujao akiwemo Mayele.

“Tunachokwenda kukifanya msimu huu ni kuongeza nguvu kidogo tu, kwenye mahitaji muhimu, niseme tu tunarudi tukiwa imara zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita. msimu ujao tutakuwa tunatangaza mafanikio mengine kama haya.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave A Reply