The House of Favourite Newspapers

ISHU YA MASTAA WENYE FIGA KONKI, MAMA ‘WAHARIBU’ MABINTI ZAO!

KILA nikiposti picha Instagram watu wanakimbilia kukomenti kuwa eti natumia dawa za Kichina ili kuongeza ukubwa wa makalio yangu. Naumia sana kuambiwa hivyo. Huwa najiuliza kwamba, kwani kila mwenye makalio makubwa ni lazima atumie dawa za Kichina?  “Kusema ukweli nimechoshwa na maneno hayo, nimeamua kumuanika mama yangu mzazi ambaye naamini shepu yangu nimerithi kutoka kwake. Huenda kwa kufanya hivi watu watanielewa,” anasema mwanadada Sasha Kassim ambaye mbali na kuwa video queen, amejipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na picha zake tata anazoposti.

Katika jamii yetu, pale ambapo mama anapata mtoto ambaye wamefanana sana, watu huwa wanasema, mama kamharibu mwanaye. Hata akifanana sana na baba yake, watasema baba kamharibu mwanaye. Ni msemo tu wa kuonesha kwamba, mtoto kakopi kila kitu kutoka kwa mzazi wake. Linapozungumziwa suala la shepu kwa mastaa, imekuwa ikielezwa kuwa, wale ambao wana makalio makubwa wengi wanatumia dawa za Kichina. Wapo waliowahi kukiri kutumia dawa hizo wakidai kwamba, wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa wanatamani ‘mipododo’ lakini Mungu hakuwajaalia, hivyo wanajiongeza.

Dawa wanazotumia wadada hao zimekuwa zikielezwa kwamba zina madhara lakini wala hawasikii, wanaiangalia sana leo ya kuwa na muonekana mzuri bila kujali kuwa kesho inaweza kuwa mbaya baada ya madhara ya dawa hizo kuanza kuonekana. Lakini wakati baadhi wakitumia dawa hizo kuongeza makalio, gazeti hili limethibitisha pasi na shaka kwamba, wapo warembo ambao shepu walizonazo ni za kurithi kwa mama zao. Yawezekana wapo wengi ambao kweli wamechukua maumbo kwa wazazi wao ila kwa kuwa mama zao hawajawahi kuonekana, wanaambiwa wanatumia dawa.

Wakati f’lani staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu aliwahi kuandamwa sana kwamba anatumia dawa za Kichina na ndiyo maana ana mkalio kama wote. Kutokana na maneno hayo, mama yake, Miriam Sepetu aliamua kuvunja ukimya na kueleza kuwa, wanaomsema mwanaye kuwa anatumia dawa za Kichina wakome maana kalio lake ni orijino na amelirithi kutoka kwake.

Ukiachana na mama Wema ambaye aliamua kumtetea mwanaye, wapo mastaa ambao ilibidi wawaanike mama zao ili kufuta zile kauli za kwamba nao wanaingia kwenye lile kapu la wale wanaotumia dawa za Kichina. 

SASHA KASSIM

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, mipicha iliyochukua nafasi ni ile inayoonesha figa yake matata. Kwa kuwa amekuwa mhanga wa kuambiwa anatumia dawa za Kichina kwa muda mrefu, hivi karibuni aliamua kuachia picha ambayo amepiga na mama yake, wakiwa wamevaa nguo zinazofanana huku shepu zao zikionekana sawia.

Ukiiangalia picha hiyo, kama wewe ni kati ya waliokuwa wakidhani mpododo wa Sasha ni wa Kichina, lazima utaona aibu. Utajiona kwamba alikuwa akizungumzia jambo usilolijua. Picha hiyo inathibitisha kwamba, Sasha kakopi na kupesti kutoka kwa mama yake mzazi aliyemtambulisha kwa jina la Fatma.

SANCHI

Jina lake halisi ni Jane Ramoy. Naye umaarufu wake ameupata kupitia mtandao wa Instagram. Ni binti asiye na aibu linapokuja suala la kuanika maungo yake. Hakuna picha mbaya ambayo hajawahi kupiga. Kutokana na kuonekana ni mrembo anayeweza kufanya lolote ili kuwashtua wanaume, naye amekuwa akiandamwa na skendo ya kutumia dawa za Kichina kuongeza kalio lake.

Mara zote amekuwa akipuuza maneno hayo lakini naye siku za hivi karibuni aliona awaumbue waliokuwa wakimfikiria tofauti kuhusu shepu yake, akaamua kupiga picha akiwa na mama yake. Wengi walioiona picha hiyo waliishia kusema; ‘huyu mama yake kamharibu kwa figa’. Hakika lishepu la Sanchi ndilo lishepu la mama yake.

POSH

Mwanadada huyu amejipatia umaarufu sana kwenye mtandao wa Instagram akifahamika kwa jina la Poshqueen. Naye ana kishepu amaizing, namba nane flani hivi lakini mpododo alionao si wa kitoto. Mdada huyu alikuja kuwa maarufu zaidi baada ya kubainika kuwa ni kati ya wanafunzi waliohitimu masomo yao mwaka huu katika Chuo cha Fedha (IFM).

Ukifuatilia comments nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusiana na shepu yake, baadhi walisema yaleyale kwamba, naye anatumia dawa za Kichina. Mapema kabisa akaona awafunge mdomo washakunaku, juzikati akatupia picha akiwa na mama yake. Watu wakaishia kusema; Waooooh! Like mother, like daughter! Walichomaanisha ni kwamba, Posh naye shepu yake ni zao la mama yake.

Makala: AMRAN KAIMA

Comments are closed.