The House of Favourite Newspapers

ISHU YA NDOA BABA AMLIPUA MKE WA NIVA!

DAR ES SALAAM: BABA mkwe wa muigizaji Zuberi Mohammed ‘Niva’, Said Kayoka amemlipua bintiye aliyeolewa na mwigizaji huyo, Maisara kwa kumueleza kuwa, hakupaswa kumuaibisha mumewe mitandaoni. Hivi karibuni, binti huyo alikaririwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na televisheni akimchana mumewe kwa mambo mengi likiwemo la kudai mumewe anapenda sana kufanya tendo la ndoa.

Mrembo huyo alienda mbali zaidi kwa kusema anaidai talaka yake kwani amechoshwa na kasumba za mumewe huyo. Kufuatia kusambaa kwa vipande vya mahojiano ya mwanamke huyo mitandaoni, Risasi Jumamosi lilimtafuta baba mzazi wa Maisara ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo ambapo alipopatikana, alipinga vikali kitendo alichofanya bintiye.

“Kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Ijumaa (Julai 27) kuhusu Maisala kumkataa mume wake, watu mbalimbali wamekuwa wakinishutumu mimi kuwa huenda ninamsapoti mtoto wangu kudai talaka kitu ambacho si kweli

“Mimi siungi mkono na sheria hairuhusu. Pia mimi kama baba mzazi sikupenda wala kuafiki kitendo cha yeye kwenda kwenye mitandao ya kijamii kuelezea hali halisi ya yeye na mume wake hata kama alikuwa anadai talaka hili suala lilikuwa lipo Bakwata, tulikubaliana ya kuwa tutalimaliza,” alisema mzazi huyo.

Akizidi kuelezea jambo hilo, mzazi huyo alisema alishangaa ghafla kumuona bintiye akifunguka mambo ya ndani kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho si sahihi hata kidogo.

“Nashangaa tu napigiwa simu na watu mbalimbali wakiwemo rafiki zangu, ndugu zangu wa Tabora naambiwa angalia mwanao maelezo anayoyaongea kwenye Shilawadu sijui, ikabidi niangalie kiukweli katika vitu alivyoviongea nilisikitika sana, vinanitia aibu mimi pamoja na familia, na kabla hapo kinachonisikitisha binti yangu aliniletea barua ya wito wa Bakwata akaniambia barua nimpelekee mkwe wangu, kisheria hakutakiwa kufanya hivyo.

“Suala hili lipo Bakwata ili kuweza kusuluhishwa kwa kuwa mimi na famila yangu hatukubali ile ndoa ivunjike, kwa hiyo Jumamosi hii (leo) inatakiwa tukutane pale, familia yangu pamoja na familia ya Niva ili tuweze kusuluhisha ndoa hiyo,” alisema Said.

Comments are closed.