The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Udhalilishaji…Makosa 3 ya Gardner kwa Jide!

0

gardner (1)Mtangazaji Gardner G. Habash.

NA OJUKU ABRAHAM

GARDNER G. Habash na Judith Wambura Mbibo bado ni stori kubwa mjini, licha ya kuwa wawili hawa waliacha kulala kitanda kimoja kama mke na mume mwezi mmoja kabla ya tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao kuanza kuvuja, yapata miaka miwili iliyopita.

Licha ya usiri wa wote wawili, hatimaye ikathibitika kuwa ndoa hiyo haipo tena, ingawa kwa muda mrefu ilipigiwa mfano wa jinsi mastaa wanavyoweza kudumu katika uhusiano, wakati ule watu maarufu walivyoshindwa kukaa kwa muda mrefu kwenye uhusiano wao.

jidenagardnerMtangazaji Gardner G. Habash na mtalaka wake, Nguli wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Jide’.

Baada ya kupeana talaka katika Mahakama ya Mwanzo Manzese jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita, wakati kila mmoja akiamini kuwa ukurasa wa wawili hao umefungwa rasmi, wimbo mpya wa Ndi Ndi Ndi wa Lady Jaydee, ukaibua upya hisia za mashabiki kuwa mashairi ya kibao hicho yamemlenga Gardner.

Na bila kutarajia, siku chache zilizopita, Gardner, akiwa katika kazi zake binafsi, alipanda jukwaani na kutoa maneno yanayotafsiriwa kama kijembe kwa mkewe huyo wa zamani, ambacho kimekuwa gumzo kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kila mmoja kwa nafasi yake, anazungumza anavyojua kuhusu watu hawa wawili. Ni kwa misingi hiyo, nami natazama makosa ya Gardner na wajibu wake kwa Jide, tukianza na makosa.

JIDELady Jaydee ‘Jide’.

JUKWAA HALIKUWA MUAFAKA

Gardner anadaiwa kutoa maneno hayo yaliyompatia jina jipya katika ukumbi mmoja wa burudani wilayani Temeke, ambako wasichana wanaoshiriki shindano moja la urembo walikuwepo.

Kutamka maneno kama aliyotamka, mbele ya wasichana wale, wengine wakiwa wadogo kuliko Jide, halikuwa jambo la busara na kwa akili za kawaida, alitaka waliokuwa mbele yake, wamdharau mkewe wa zamani.

Angeweza kupeleka ujumbe kama aliotaka kuufikisha, kwa kutamka maneno yenye staha kama vile “Sina matatizo na yule mtoto wa kike, ndani ya miaka 15, nimemfahamu vizuri sana”

MANENO YALIKOSA UHALALI

Kila aliyesikiliza na kuona kipande kile cha video, atakubaliana nami kuwa hakuna sehemu ambayo Gardner alitukana, isipokuwa kauli aliyoitoa, kwa watu waliostaarabika, haikustahili. Kwanza kwa kuwa waitikiaji wake walikuwa wanawake na pia maudhui hayakuwa muafaka.

Angeweza kutumia maneno yaleyale, akiwa amekaa na wanaume wenzake, wala isingechukuliwa kama ni udhalilishaji, bali ingeonekana kuwa ni mtu anayejisifu, kwamba yeye ni kidume.

WAKATI NAO HAUKUWA MUAFAKA

Unapoitazama video ile, unatambua kuwa ni usiku. Unapomtazama Gardner vizuri, unashawishika kuamini kwamba alikuwa tayari ameshapata ‘yale mambo yetu’ hivyo kumfanya ajisikie huru kutamka maneno ya kuufurahisha moyo wake.

Ninaamini endapo ingekuwa muda wa kazi wa kawaida, kwa vyovyote angekuwa mwangalifu katika kujibu au kusema jambo lolote linalomhusisha mtalaka wake kama ambavyo kwa kipindi chote cha mgogoro wao, alivyokuwa makini.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply