The House of Favourite Newspapers

Islamic States Yathibitisha Kuhusika na Shambulio katika Mji wa Lume, DRC

0

KUNDI la kigaidi la Islamic State limethibitisha kuhusika kwenye shambulio la siku ya Alhamisi ambalo lililenga mji wa Lume, jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa ujumbe wa shirika la habari la kundi hilo.

 

Kundi hilo limedai kuhusika kupitia taarifa yao iliyotolewa kwenye mtandao wa Telegram bila kutoa maelezo zidi.

 

Siku ya Ijumaa, mashahidi wawili walisema washambuliaji waliwaua zaidi ya watu 12 katika zahanati moja, na kusema uvamizi huo ulitekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu wanaoshirikiana na Islamic State.

 

Kundi hilo lilishambulia kliniki inayoendeshwa na kanisa katika majira ya saa nne usiku wa Alhamisi.

 

Msemaji wa jeshi Alinukuliwawa akisema kwamba washambuliaji hao wanatoka katika kundi ambalo linashirikiana na kundi la ADF na kwamba walikuwa wanatumia mbinu zinazowiana na zile zinazotumiwa na kundi hilo la ADF.

 

Jeshi liliwaua wapiganaji hao watatu na kumkamata mmoja baada ya kujibu shambulizi hilo katika mji wa Lume, alisema msemaji wa jeshi Antony Mualushay.

 

Leave A Reply