The House of Favourite Newspapers

Messi Atishia Kuondoka PSG Endapo Klabu hiyo Itamsajili Cristiano Ronaldo

0
Staa wa klabu ya Paris Saint-Germain, Lionel Messi

RIPOTI zinaeleza kuwa, staa wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi, ametishia kuondoka kikosini hapo endapo klabu hiyo itamsajili Cristiano Ronaldo.

 

Kwa sasa Ronaldo anatajwa kuondoka Manchester United, huku PSG ikiwa ni kati ya timu ambazo zinatajwa kumuwania sambamba na Chelsea na Bayern Munich.

 

Imeelezwa kuwa, hakuna uhakika kama PSG itatishika na suala hilo la Messi kwani timu hiyo inataka kujipanga kuona inafanya kweli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Staa wa Klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo

Lakini imeelezwa kuwa, uwepo wa Kylian Mbappe kwenye projekti mpya kunaweza kumvuta Ronaldo ndani ya kikosi hicho, Messi na Ronaldo wamekuwa washindani wakubwa kwenye soka ambapo wanatajwa kuwa ni wachezaji wenye rekodi za kutisha.

 

Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye Ballon D’or nyingi akiwa nazo tano, huku Messi akiongoza akibeba saba.

 

Leave A Reply