#GlobalCelebrityUpdates: Itazame Movie Trailer Ya ‘All Eyes On Me’ Inayosimulia Maisha Ya Tupac Shakur – (Video)

Kwa wale mashabiki wa TuPac Shakur na muziki wa Hip Hop kwa ujumla pokeeni official movie trailer ya ‘ All Eyes On Me’ inayosimulia maisha ya rapper huyo.

‘All Eyes On Me’ ni movie inayosimulia maisha halisi ya aliyekuwa mmoja wa rappers wakubwa duniani Tupac Shakur(2Pac) 

Filamu (Biopic) hii itawapa fursa watu na mashabiki wa TuPac pamoja na mashabiki wa muziki wa Hip Hop kwa ujumla kuona stori ya maisha ya rapper huyo aliyekulia New York, Marekani , sababu zilizomsukuma kujihusisha na muziki wa Hip Hop, beef lake na rapper Notorious B.I.G na mengine ikiwemo  kifo chake akiwa na umri wa miaka 25 tu. Muongozaji wa Biopic hii anaitwa Benny Boom, huku muhusika mkuu wa filamu hiyo anaitwa Demetrius Shipp Jr. ambaye ndiye aliyeuvaa uhusika wa Tupac Shakur.

‘All Eyes On Me’ itaanza kuchezwa kwenye nyumba za sinema duniani kuanzia tarehe 16 June 2017, tarehe ambayo TuPac Shakur angekuwa anatimiza miaka 46.

 ALL EYES ON ME‘ (2017 MOVIE) BASED ON TUPAC SHAKUR

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Video: YouTube/ CODE Black Films.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

 

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment