The House of Favourite Newspapers

Itel Yawakumbuka Watoto Wenye Uhitaji Maalum, Yawasapoti Kimasomo

0
Meneja Uhusiano wa itel Tanzania Fernando Wolle akigawa vifaa kwa wanafunzi wa Shule ya Ubungo NHC.

 

 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya itel Tanzania leo Aprili 29 mwaka 2022 imerudisha fadhila kwa jamii kwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji maalum wa Shule ya Msingi Ubungo National Housing, Dar.

Meneja Masoko wa itel Tanzania, Elphas Wilbert akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo shuleni hapo.

 

 

Akizungumza na wanahabari Meneja Mahusiano wa Itel Tanzania, Fernando Wolle amesema;

“Leo tumetembelea hapa Shule ya Msingi Ubungo NHC kwaajili ya kuweka nguvu zaidi katika kuendeleza elimu, sote tunafahamu serikali inafanya jitihada kubwa sana kuendeleza miundombinu ya elimu ikiwemo kujenga madarasa kutokana na ongezeko la idadi kubwa ya watoto.

Watoto wakifurahia na mabegi waliyopewa.

 

 

“Hivyo nasi tumeona tuunge mkono jitihada za serikali kwa kutoa vifaa vya masomo. “Lakini kwa kifupi ni kwamba itel ilianzisha kampeni ya CSR yenye kauli mbiu ya Love Always On’ yaani Upendo Usiozima tangu mwaka 2003 ikilenga kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia wanafunzi na watoto kuwa na mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi vya shuleni.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo NHC, Paulo Mdachi akitoa shukrani zake baada ya shule yake kukabidhiwa misaada hiyo.

 

 

“Hakuna asiyefahamu kuwa watoto ni hazina na ni taifa lijalo hivyo sisi itel kwa kutumia kauli mbiu yetu ya “Enjoy Better Life” tunahakikisha tunatengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kutimiza azma yetu ya kuwasaidia watoto kufurahia maisha bora.

 

“Progamu hii kwa sasa inatekelezwa nchi zote za Afrika ambazo itel inapatikana. Kwa upande wa Tanzania itel imeshafanya matukio ya kurudisha fadhila kwa jamii yaani CSR mara kadhaa katika shule na vituo vya kulelea watoto yatima tangu mwaka 2016 mpaka sasa.

“Pia tumeanzisha mradi wa maktaba unaojulikana kama ‘Wandering Libraries Project’ tangu 2021 na huu utakuwa ni mradi wa muda mrefu wa CSR wa itel. Lengo ni kuchangia maktaba ndogo zaidi ya 10,000 kote barani Afrika katika miaka mitatu ijayo.

 

“Hivyo basi kama ilivyopendekezwa hapo awali tumetembelea shule hii kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaolelewa katika mazingira magumu au familia zenye kipato cha chini ya mstari kwa kuwapatia vifaa vya masomo yakiwemo mabegi, madaftari, kalamu, chupa za maji na miamvuli iwakinge na mvua hususan kipindi hiki ambacho masika yanaendelea.

 

“Pamoja na msaada huu kwa watoto hawa wanaoishi katika mazingira magumu, pia itel Mobile Limited tumeipatia shule hii ya Ubungo NHC shelfu 20 za kuhifadhia vitabu pamoja vitabu vya kiada 217 kwa masomo ya sayansi, hesabu na kiingereza kwa darasa la tatu, la nne na la tano.

 

“Msaada huu kwa pamoja una thamani ya shilingi za kitanzania milioni tano na zoezi hili ni endelevu hivyo tunawakaribisha wadau wengine kushirikiana nasi na kuendeleza elimu hapa nchini Tanzania.” Alimaliza kusema Meneja Mahusiano itel Tanzania Fernando Wolle ambaye aliambatana na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Elphas Wilbart.

 

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo, Paulo Mdachi ameishukuru kampuni hiyo na kuziomba taasisi zingine kuiga mfano wa itel ili tuweze kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Leave A Reply