The House of Favourite Newspapers

Iyanya azungumzia uhusiano wake na Freda Francis

Iyanya-and-Freda-FrancisMwanamuziki Iyanya akiwa Freda Francis.

BAADA ya kuvuma kwamba anatoka na Yvonne Nelson ambaye ni mcheza sinema maarufu wa Ghana, mwanamuziki Iyanya wa Nigeria, aliamua kuyafanya siri mahusiano yake mengine na kina dada.

Hata hivyo, alipogundua uvumi unaendelea mitaani kuhusu ‘washikaji’ wake wa kike, mwimbaji huyo aliamua kuweka ukurasa wake wa Instagram picha inayomwonyesha akiwa na Freda Francis, mkuu wa kampuni la Global Orchard Service and Oasis Med Spa.

Alihojiwa katika kipindi cha Breakfast Club cha televisheni ya DZRPT, Iyanya alifunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na Freda Francis.

“Siwezi kusema kama nina uhusiano na Freda au la, sitaki kujiingiza katika matatizo. Nikilijibu swali hili sasa itabidi nijibu maswali mengi zaidi, hivyo sitalijibu. Isitoshe, mashabiki wangu wanachojali ni muziki wangu na si nani mpenzi wangu,” alisema.

Iyanya ambaye ni mwenyeji wa Jimbo la Cross River, alikiri kwamba mashabiki wake wa kike wanamsumbua kwa kumtumia picha zinazoonyesha matiti yao.

“Ndiyo, mashabiki hawa si waoga. Nimeyaona matiti yao kwenye picha nyingi na mambo mengine ya kuvutia. Nina mashabiki wengi wa kike wenye mizuka ambao wanataka mwili wangu tu na si muziki wangu (anacheka).”

Comments are closed.