The House of Favourite Newspapers

Jahazi Kuitambulisha Albamu mpya Dar live

0

jahazi+PICMwandishi Wetu,
Dar es Salaam

KUNDI la muziki wa Taarab, Jahazi Modern, linatarajiwa kutambulisha albamu yake ya Kaning’ang’ania Ng’ang’anu, Machi 12, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo, alisema usiku huo Jahazi wakiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf, wataporomosha nyimbo zao zote kali zilizobamba na zinazoendelea kubamba.

“Jahazi inawajali wapenzi wake wa burudani, hasa wale wanaopenda kiwanja cha Dar Live, baada ya kuizindua Albamu ya Kaning’ang’ania Ng’ang’anu, sasa itaporomosha nyimbo zote zilizoimbwa na wakali ambao ni Mwanakhamis Mohamed ‘Miss Jahazi’, Fatuma Kassim, Leila Rashid pamoja na Fatuma Ally,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi 8,000 tu getini.

Leave A Reply