The House of Favourite Newspapers

Jaji Mkuu Amshauri Kenyatta Kuvunja Bunge, Spika Agoma!

0

JAJI Mkuu wa Kenya, David Maraga, ameeleza kuwa atamshauri Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kuvunja bunge la nchi hiyo baada ya kushindwa kupitisha sheria inayowatambua watu wanaozaliwa na jinsia mbili.

 

Katika barua kwa Kenyatta, jaji huyo alisema kwamba kushindwa kuwa na wabunge wengi wa kike ni ukiukaji wa katiba na ubaguzi dhidi ya wanawake.

 

Maraga katika hatua yake ambayo haijawahi kutokea hapo awali, amesema kwamba bunge limekataa kufuata agizo la Mahakama Kuu la kutunga sheria inayotambua watu wenye jinsia mbili kwa zaidi ya miaka tisa.

 

Katiba inasema kwamba jinsia moja haiwezi kudhibiti zaidi ya theluthi mbili ya viti vya bunge. Hata hivyo, wanawake wana viti vichache ikilinganishwa na viti 116 vinavyohitajika katika bunge hilo la wabunge 350.

 

”Bunge limeshindwa ama kupuuza sheria zinazohitajika kuidhinisha sheria hiyo ya jinsia, licha ya maagizo manne ya mahakama.

 

“Haiwezekani kwamba Bunge halijatii agizo la Mahakama Kuu katika maombi ya kikatiba No. 371 ya 2016 kwa zaidi ya miaka tisa sasa,  bunge halijatunga sheria inayohitajika kutekeleza sheria ya jinsia mbili ambayo, kama korti ya rufani ilivyozingatia katika uamuzi wake,  ni dhahiri bunge halijali mtazamo kuhusu jambo hili.

 

“Ikiwa Bunge litashindwa kutunga sheria kwa mujibu wa agizo chini ya kifungu cha (6) (b), Jaji mkuu atamshauri rais avunje bunge; ni jukumu langu kikatiba kukushauri Rais wa Jamhuri ya Kenya, ” alisema Maraga.

 

Lakini akimjibu, Spika wa Bunge, Justin Muturi, alisema kwamba kuvunjwa kwa bunge ni chaguo lisilowezekana. Katiba mpya ya Kenya ilizinduliwa 2010, na sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili ilibidi kuidhinishwa baada ya miaka mitano.

 

Huku kukiwa kumekuwa na mjadala kuhusu suala hilo, bunge hilo lenye wanaume wengi halijapata mbinu ya kupata wanawake wengi bungeni, huku baadhi ya wabunge hao wakihoji dhidi ya kubuni viti vingi hususan vya wanawake na badala yake kuwataka wanawake kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge mashinani.

 

”Hatuwezi kusahau kuhusu changamoto zinazotukabili tunapojaribu kuidhinisha suala hili na kuligeuza bunge kuwa eneo la kupigania usawa wa jinsia,” alisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

 

Aliongeza kwamba bunge la 10 halikuwa na muda wa kutosha kuidhinisha sheria inayohitajika kuhalalisha sheria hiyo ya jinsia. Kulingana na Maraga, mahakama ya upeo chini ya aliyekuwa Jaji Mkuu, Willy Mutung, iliagiza bunge kuidhinisha sheria hiyo kufikia tarehe 27 Agosti 2015.

 

Jaji huyo alisema kwamba pingamizi kadhaa ziliwasilishwa mahakamani zikilitaka bunge kuidhinisha sheria hiyo.

 

”Hata hivyo, bunge lilishindwa kuidhinisha miswada iliowasilishwa mbele yake”.

Leave A Reply