The House of Favourite Newspapers

Jaji wa serikali kuu anayesimamia kesi ya Trump aamuru mawakili wake kufika mahakamani Ijumaa

0

TRUMPTRUMP

Waendesha mashitaka walisema wanapatikana wiki nzima, huku mawakili wa Trump wakiomba kuahirishwa hadi mapema wiki ijayo.

Jaji wa serikali kuu anayesimamia kesi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuhusu mashtaka ya kujaribu kubatilisha uchaguzi wa mwaka 2020 ameamuru mawakili wake na waendesha mashtaka wa serikali kuu kufika mahakamani siku ya Ijumaa kwa ajili ya kusikilizwa ili kusaidia kubainisha jinsi ushahidi unaweza kutumika na kushirikishwa katika kesi hiyo.

Jaji wa Mahakama ya wilaya Tanya Chutkan alipanga kusikilizwa kwa kesi hiyo Ijumaa saa 4 asubuhi saa za Washington muda mfupi baada ya mawakili wa Trump na wajumbe wa ofisi ya Wakili Maalum wa Marekani Jack Smith kutofautia na juu ya wakati wa kupanga shauri hilo.

Waendesha mashitaka walisema wanapatikana wiki nzima, huku mawakili wa Trump wakiomba kuahirishwa hadi mapema wiki ijayo.

KIVUMBI KINAANZA LEO NGAO ya JAMII/ MASTAA WAPYA WATAMBIANA/ KOCHA SIMBA ATUMA SALAMU…

Leave A Reply