The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-4

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Moyoni nilimsifu kaka Cheni, yaani mchana yule, usiku huyu tena! Loo! Niliamua kulala mapema ili nisisumbuliwe na mambo yao yatakapoanza. Niliwakadiria wataanza mechi baada ya kama nusu saa za kusaka stimu kwanza kwa maongezi, kumbe weee..!
SASA TAMBAA KIVYAKO…

Nilisikia bwana! Bwana nini? Moyoni nikasema tayari. Niliziba masikio ili nisiwasikie wanachoendelea nacho lakini mwili nao umeumbwa kutamani. Nilijikuta natoa vidole ili nisikie japo kidogo na kwa mbali.

Nikasikia sauti za kuhema kwa kaka Cheni huku huyo mwanamke akishadadia kwa sauti nyembamba za mahaba bila kujali Cheni yupo nyumbani kwa baba yake na mama yake mzazi.

Niliamka nikakaa, ndiyo ikawa tabu zaidi. Mwanamke kama aliambiwa kwamba chumba cha pili kuna mimi. Maana alikuwa akipiga kelele utadhani anacheza sinema sasa anafanya makusudi kuongeza mbwembwe ili sinema iwe nzuri.

Ilifika mahali ikawa waziwazi, kwamba sauti za wote zikawa juu…juu zaidi! Mwanamke alisema maneno yote moja kwa moja bila kuchengesha. Yaani nilimsikia akimwambia kaka Cheni kile alichotakiwa kufanyiwa, kuongezewa au kufanya yeye.

Ili kuwakatisha au kuwafanya wapunguze spidi au manjonjo, nilikohoa kwa sauti ya juu lakini kavu. Haikusaidia kitu kwani ilionesha hata kukohoa kwangu wao walikuchukulia kama ni sehemu ya mapenzi yao.

Nilitoka kitandani, nikafungua mlango nikiwa na kanga moja tu, nikatoka nje. Hali ya hewa ilikuwa ya joto hivyo kutoka kwangu nje nilihisi kungesaidia kupata upepo.

Lakini kama nilivyosema, moyo umeumbwa na tamaa ya kupenda kusikia au kuona vitu vibaya na vizuri pia. Eti pamoja na kukaa nje, nikawa sina amani moyoni. Nikatamani kurudi ndani eti nikasikie wapo kwenye hatua gani muda huo.

Tena mbaya zaidi, ukitaka kuujua moyo kwamba siyo, wakati nataka kwenda ndani, moyo ukawa unalaani kwa kusema ‘ngoja nikawasikia hawa wazinzi, wasiokuwa na haya, muda huu wamemaliza au bado?’ Lakini najua moyo wangu ulitekwa na shetani ili nikashiriki na mimi na kuendelea kupata msisimko.

Basi, niliingia ndani. Nikasikia kama vile ndiyo kwanza wanaanza halafu kama vile kila mmoja wao alikuwa hajakutana kimwili na mwenza wake kwa miezi sita.

Mwanamke alikuwa akimuita kaka Cheni kwa jina kama wimbo. Analiita, kaka Cheni akiitika hamwambii lolote, anaita tena. Ikawa hivyohivyo mpaka akabadili sasa, akamwambia kisa cha kumuita, nikajua kumbe ndiyo maana alikuwa anamuita sana.
Hapo tena nikamsikia mwanamke akimjulisha kaka Cheni kwamba amefikia wapi yeye, kaka Cheni naye akamwambia amefikia wapi.

Mimi pale kitandani, licha ya kuwa peke yangu, nilihangaika sana kujiridhisha, kwani biti zilikuwa zinapigwa kwingine, mimi naambulia kucheza. Nililala chali, nikanyoosha miguu, nikawa najishika nido, najipapasa sehemu ya kifua, nafumbua macho na kuyafumba kwa wakati huohuo.

Nikaja kuwasikia kila mmoja akimjulisha tena mwenzake alipofikia, kumbe wote walikuwa wanafika sehemu hiyo pamoja. Nilijitahidi sana na mimi nikafika sehemu hiyohiyo kama wao. Tukafika wote. Nilichoka sana, nikatupa mikono na miguu huku na kule. Mwili wote ulikuwa hauna nguvu.

Sijui nini kiliendelea, nilipitiwa na usingizi moja kwa moja na kuja kushtuka saa kumi usiku nikiwa napitisha kumbukumbu kichwani, nikakumbuka mara ya mwisho ilikuaje. Nikakumbuka nilifikia sehemu moja na kaka Cheni na mwanamke wake, nikakasirika sana.
***
Asubuhi ilifika, kulikucha, nikatoka kufanya kazi za ndani uani huku nikiwa nalenga kuona kama yule mwanamke wa kaka Cheni aliondoka au alilala palepale. Nilifanya kazi kwa umakini wa macho. Muda mwingi nilikuwa nakazia macho mlangoni kwa kaka Cheni.

Saa moja, kaka Cheni alifungua mlango wake. Akatoka yeye akiwa amevaa bukta nyeusi tu, juu alikuwa kifua wazi. Akakutana macho na mimi, akaachia tabasamu. Mimi nilihisi aibu, nikaangalia pembeni, moyoni nikasema; ‘kaka Cheni bwana’.
“Mama ameamka?” aliniuliza.

“Kaenda kwenye maji,” nilimjibu nikiendelea kuangalia pembeni.
“Hujanijibu swali. Nimekuuliza mama ameamka, unajibu kaenda kwenye maji.”
“Sasa kaka Cheni anaweza kwenda kwenye maji akiwa amelala?” nilimjibu ki hovyo maana hata yeye alijua kwa nini nilimjibu vile.
“Yamekwisha…kwenye maji wapi?”
“Kwa mama Tabu.”

Kaka Cheni akarudi chumbani kwake. Nikajua kwa nini aliniuliza vile. Nikajua alilala na yule mwanamke wake sasa alitaka kujua alikoenda mama ili amtoe mwanamke wake.

Baada ya dakika tatu, kaka Cheni alitoka akiwa amevaa traki suti, nyuma yake akafuatiwa na mwanamke. Jamani! Ninaposema mwanamke nieleweke kwamba ni mwanamke. Sijui kama Cheni alimpendea nini maana si saizi yake. Muwowowo huo, mpaka nikacheka mwenyewe moyoni.

Nikasema loo!
Akitembea sasa, mbengenyu… mbengenyu…mbengenyu. Hapo alikwenda chooni. Akiwa bado chooni, baba akatoka na kiti, akakaa nje…

Nilimwona kaka Cheni akishtuka sana. Hata mimi nilishtuka kwani nilijua baba ameshakwenda kazini kwake, kumbe alikuwepo bwana.
“Shikamoo baba,” kaka Cheni aliamkia huku wasiwasi wake ukiwa umegundulika na baba.

Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma kwenye gazeti hilihili, wiki ijayo.

Comments are closed.