The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-6

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Anko, Mwanamaua anasema amesahau kitambaa chake cha kichwani chumbani kwako kitandani, kasema nipe nimpelekee ataulizwa na mama yake asiporudi nacho…halafu kasema hujamwambia usiku wa leo aje au asije maana simu yake ina matatizo ya chaja.”
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…

Nilimwona baba akitetemeka, akamkazia macho kaka Cheni, akasimama maana alikaa…
“Cheni,” aliita mama akitoka ndani na si baba…
“Abee…” kaka Cheni alichanganyikiwa, ilibidi aitike kama mwanamke, kama binti…
“Bee nini? Bee wewe mwanamke?” mama alimjia juu…
“Naam mama…”

“Mwanamaua ni nani?” aliuliza baba akiwa bado amesimama…
“Dada mmoja tunafahamiana.”

“Kitambaa chake alichokisahu kimefikaje kitandani kwako?”
“Alikuja jana jioni akakisahau alipotoka.”
“Alikuja jana jioni hapa?”
“Ndiyo baba.”

“Kumbe wewe wanaokuja kwako si wanaume, ni wanawake siyo? Nikisikia umempa mtoto wa watu mimba, Cheni utanibeba bila mbeleko ya kijani,” alisema baba na kuingia ndani.

Nje tukabaki mimi, mama na kaka Cheni mtuhumiwa. Mama akaanza…
“Hivi we Cheni kwanza mimi naomba kukuuliza…wewe unafanya kazi gani usiku mpaka unashindashinda ndani mchana kutwa umelala?”
“Sina kazi mama, sasa nitakwenda wapi?”

“Ndiyo ushinde ndani umelala kitandani?” mama aliuliza tena, nikamwona kaka Cheni akinikazia macho mimi. Nikainamia chini kwa aibu…
“Dada yako ndiyo anayekusaidia kulala ndani mchana kutwa? Maana naona unamwangalia,” alisema mama, ikabidi mimi nicheke kidogo.

Kifupi maneno ya mama yaliashiria kwamba, hapendezwi na kitendo cha kaka Cheni kulala tuuu…mpaka giza linaingia ndiyo anatoka kwenda kutembea. Na hii ndiyo ilikuwa kawaida yake. Mbaya zaidi sasa, akitoka usiku kwenda kutembea, akirudi ndiyo amebebana na akina Mwanamaua, mara Consolata, mara Jemina yule mtoto wa mzee Ukawa.

Wakati wote huo, yule mtoto aliyetumwa kitambaa alishaondoka nyumbani tena kwa kukimbia. Nadhani alipeleka taarifa kwa Mwanamaua kwamba kimenuka!
Mama aliendelea na shughuli zake, baba akatoka kwenda zake wapi sijui. Kaka Cheni aliingia kuoga, alipotoka alivaa akaniaga anakwenda kuzurura, nikijua anayafanyia kazi maneno ya mama.

Ilipita saa tatu, saa nne, saa tano, saa sita, saa saba, saa nane, kaka Cheni akanipigia simu…
“Halo sista…”
“Niambie my braza.”

“Mmeshapika?”
“Yes! Tumekuwekea chakula, mama amekwenda kwenye msiba wa mzee Timo.”
“Dingi?”
“Dingi hajarudi, lakini mama alisema naye atakwenda hukohuko msibani na watalala hukohuko leo.”

Kaka Cheni alikata simu. Baada ya dakika kumi tu, akatokea. Safari hii alikuwa na msichana mwingine kabisa, mgeni machoni pangu.

Kusema kweli hapo kaka Cheni akiamuaga kuchagua utamkubali. Huyu msichana aliumbika jamani! Kila sehemu ya mwili wake ilikuwa ya wastani. Wowowo la wastani. Miguu ya wastani, kiuno cha wastani, macho ya wastani. Kila kitu ni wastani. Nilipapenda zaidi kifuani pake. Palikuwa panalipa!

“Suu, huyu ni sista ‘angu,” kaka Cheni alimtambulisha, akaniangalia mimi…
“Sista huyu ni wifi yako wa ukweli kabisa.”
“Hata mimi namwona, karibu wifi ‘angu,” nilimwambia.
“Asante sana wifi.”

Waliingia chumbani. Baada ya muda, kaka Cheni akanitumia meseji kwamba anaomba nimwingizie msosi wake ndani. Nikafanya hivyo.
Kwa sababu nilikuwa sina kazi, baada ya kumwingizia chakula na maji ya kunawa na ya kunywa na matunda, niliingia chumbani kulala.

Niliwasikia wakila huku wakizungumza mambo ya kimahaba zaidi. Wakati fulani niligundua kuwa, hapo Suu anamlisha kaka Cheni au hapo kaka Cheni anamlisha Suu.
Sasa nikaja kubaini kuwa, wameshamaliza kula, wanachombezana, maana nilisikia Suu akisema…

“Cheni nini bwana…subiri…aaa Cheni wewe…sasa huko nako nini?”
Mara nikasikia ukimya tuliii. Halafu ghafla nikamsikia Suu akihema kwa kasi na kusema kimahaba, nikajua tayari.

Nililala mlalo wa kuwaunga mkono, nikawa najipapasa na mimi katika kila hatua yao…nikafumba macho, nikafumbua, nikahisi giza, nikachezacheza kitandani.
Mara, nikasikia simu ikiita, nikamsikia Suu akiongea…

“Eee…nani? Kaanguka? Nakuja…nakuja sasa hivi,” alisema Suu na nikasikia kitanda kikilia, kuashiria anatoka kitandani. Nikachukia sana maana na mimi nilikuwa pazuri.
Suu alifungua mlango huku akimwambia kaka Cheni…
“Baby acha niende tu. Nitarudi baadaye…”

Je, unajua nini kiliendelea huko? Usikose kusoma kwenye gazeti hilihili, wiki ijayo.

Leave A Reply