The House of Favourite Newspapers

Janet Jackson Ajifungua Mtoto wa Uzeeni

janet_jackson_na_mumewe_wissam_-al-manaMwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Janet Jackson mwenye umri wa miaka 50 sasa, amejifungua mtoto mvulana bila matatizo.

Janet na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto mvulana kwa jina Eissa Al Mana.

Tetesi za mimba ya staa huyo zilianza kusambaa mwezi Aprili mwaka jana alipoahirisha ziara yake ya kutumbuiza ya Unbreakable.

jackson-janet-4fac4b9d9753f

Alisema alitaka kuangazia kuunga familia na mumewe, ambaye walifunga pingu za maisha mwaka 2012 na imeelezwa hivi karibuni ameonekana akinunua nguo na vitu vingine vya kutumiwa na watoto London.

janet-jackson-2016-thatgrapejuice-600x739

Wasifu: Janet Jackson

  • Janet Damita Jo Jackson alizaliwa 16 Mei 1966 mjini Gary, Indiana
  • Ndiye mtoto wa mwisho miongoni mwa watoto tisa wa familia yake akiwa ni dadake nyota wa muziki wa Pop marehemu Michael Jackson
  • Aliachia albamu yake ya kwanza, Janet Jackson, mwaka 1982
  • Ana jumla ya albamu11 na mwaka juzi aliachia albamu yake ya mwisho, Unbreakable.
  • Ameshinda tuzo za Grammy mara saba
  • Alianza kwa kuigiza kipindi cha maisha ya uhalisia cha familia kwenye runinga cha The Jacksons mwaka 1976. Ameigiza katika filamu kadha ikiwemo ya Tyler Perry ya Why Did I Get Married
  • Kwa sasa anaishi na mumewe wa tatu, bilionea wa Qatar Wissam al-Mana, waliyefunga naye ndoa 2012
  • Ndoa zake za awali ni ya mwaka mmoja na mwanamuziki wa soul James DeBarge imiaka ya 1980 na kwa mcheza densi Rene Elizondo Jr kuanzia 1991-2000

Janet Jackson ndiye mtu mashuhuri pekee aliyejifungua mtoto akiwa na umri mkubwa.

Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry alijaliwa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47 miaka mitatu iliyopita.

Na mke wa John Travolta, Kelly Preston, alijifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.

Nchini India hata hivyo, kuna wanawake watatu ambao wamedaiwa kujifungua watoto wakiwa na zaidi ya miaka 70.

Comments are closed.