The House of Favourite Newspapers

Janga Atoboa UVCCM Sengerema

0

Baraza kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi – CCM (UVCCM) wilaya ya Sengerema mkoa Mwanza limempitisha kwa kauli moja Ramadhan Janga kuwa katibu hamasa na chipukizi wilaya ya Sengerema.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema, Patrick Mundeba aliwashukuru wajumbe wa baraza kuu kwa kumpitisha Ramadhaman Janga kuwa katibu hamasa mara baada ya kutoa mapendekezo yake kwenye kikao hicho.

“Nawashukuru kwa kuoana anafaa kuwatumikia naomba tuungane kwa pamoja kuijenga jumuiya yetu,” amesema Mundeba.

Kwa upande wake Ramadhan Janga mara baada ya kupitishwa na baraza kuu la umoja huo kuwa katibu hamasa amewashukuru wajumbe hao na.kuahidi kuwapatia ushirikianonwa dhati.

Leave A Reply