The House of Favourite Newspapers

Janjaro Akamatika Kwa Queen Linah

0

STAA wa Hip Hop Bongo, Abdulaziz Chande ‘Janjaro’ anafunguka kuwa, hisia za kimapenzi alizonazo kwa mpenzi wake wa sasa, Linah Honnah ‘Queen Linah’ ni kutokana na kukamatika kwake na ndiye mwanamke wa maisha yake.

 

Janjaro ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, upendo alionao kwa mpenzi wake huyo haulezeki kwani kuna muda anatamani hata awapigie simu maeksi wake awaambie jinsi alivyo na furaha.

“Nashindwa niongee nini, lakini ni ukweli usiopingika kwamba sasa hivi nimekamatika, tena nimekamatika haswaa, huyu mwanamke ananipa kila ninachokitaka, heshima, mapenzi ya dhati na vitu vingine vingi ambavyo sisi wanaume huwa tunavipenda kutoka kwa wapenzi wetu, kiasi kwamba najuta kwa nini sikumjua mapema,” anasema Janjaro ambaye anakimbiza na albam yake ya Asante Mama.

STORI: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply