The House of Favourite Newspapers

Poshy: Kuzaa Hakuharibu Usichana

0

MREMBO mwenye figa la aina yake Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’, anasema kuwa, uzazi haujamfanya aharibike, zaidi ndiyo anaendelea kuwa kama msichana mdogo ambaye hata leba haijui.

 

Akipiga stori mbili-tatu na IJUMAA SHOWBIZ mrembo huyo ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Nova anasema kwamba, siku hizi mambo yamebadilika; yaani mwanamke akizaa hazeeki kama ilivyokuwa huko nyuma, kwa hiyo warembo waache kuogopa kuzaa.

“Unajua zamani kulikuwa a dhana kwamba mwanamke akizaa, basi anachoka, mara anachakaa na ndiyo maana wasichana wengi walikuwa wanaogopa kubeba mimba, lakini siku hizi hakuna hayo mambo, vitu vimebadilika sana, mwanamke akishajifungua, kuna namna nyingi za kujitunza na mwili kurudi kama ulivyokuwa awali, kama mnavyoniona mimi, mtu akiniangalia utadhani sijawahi kuingia leba,” anasema Poshy ambaye ni shosholaiti maarufu kwenye mitandao ya kijamii.

Leave A Reply