The House of Favourite Newspapers

Jay Z Amuangukia Beyonce, Amchana Kanye West

0

Huku mwanamuziki mwenye jina kubwa na mkwanja wa maana, Jay Z akisherehekea kupata watoto mapacha na mkewe, Beyonce, hatimaye ameamua kutoa albamu aliyoipa jina la 4:4 ambapo humo ndani sasa amempa makavu mshikaji wake, Kanye West na kumuomba msamaha mke wake.

Si unajua mwaka jana washikaji walikuwa kwenye ziara yao ya Watch The Throne pamoja, sasa kwenye hiyo albamu, ndani ya traki ya Kill Jay Z, mwana amemlalamikia sana Kanye West mpaka kwa kusema kwamba alimfanya mshikaji kupokea dola Milioni 20 lakini cha ajabu alimpa dakika ishirini tu kwenye stage.

Achana na hiyo, kwenye albamu hiyohiyo kuna ngoma inaitwa Moonlight ambayo ameipa jina baada ya muvi ya Moonlight ya mwaka huu ambayo inaonyesha maisha ya watu weusi na wengine wakifanya mambo ya kishoga, japokuwa muvi ilikuwa kali lakini ilitoswa kwenye Tuzo za Oscar na kupewa La La Land kitu ambacho kwake aliona kama ubaguzi ndiyo umetumika.

Filamu ya La La Land na Moonlight

Kwenye ngoma yake ya Family Fued pia aliimba kama kuizungumzia familia yake, kumuomba msamaha mke wake, Beyonce kwa kashfa za kujigijigi nje ya ndoa kitu ambacho kilimfanya mke wake huyo kulia kila siku.

Watu wametoa mawazo yao mengi huku wengi wakisema kwamba jamaa ameamua kumuomba msamaha mke wake kupitia albamu hiyo baada ya mkewe huyo kutoa Albamu ya Lemonade ambayo imezungumzia sana kuhusu mapenzi ambapo mwanaume anaweza kutoka nje ya ndoa, akaenda kujirusha na wanawake wengine huko.

Wapo wasanii wengi walioshirikiana katika baadhi ya nyimbo kwenye albamu hiyo wakiwemo Frank Ocean, Damian Marley na wengine kibao.

 

Na: Nyemo Chilongani, (GPL)

 

Leave A Reply